Mwanaume
anaweza kuongeza ladha ya mahaba kwa mke wake pale anapokuwa makini na
suala la jiografia na ustadi wakati wa tendo la ndoa.
Wanawake
ni viumbe ambao mara nyingi huwa distracted na mazingira waliyopo
kuliko wanaume hasa linapokuja suala la faragha na usalama.
Wanawake
huathirika zaidi na mazingira hasa sauti au kelele na harufu kuliko
wanaume (mume) wakiwa sita kwa sita, mfano hofu ya kwamba watoto
watasikia hasa kama watoto wanapiga kelele,hofu ya kusikiwa na majirani
au wapiti njia, hofu ya mlango kuwa haujafungwa (komeo) nk.
Mume
mmoja alisafiri kwenda nchi za mbali na aliporudi nchini kwake na
kupokelewa na mkewe walienda moja kwa moja nyumbani kwao na kwa kuwa
hakukuwa na watoto au mtu mwingine bali wao wenyewe tu, wakaamua kwa
raha zao wapeane zawadi ya miili yao kwanza kabla ya lolote kwa kuwa
walikuwa na hamu kubwa kila mmoja kwa mwenzake, hata hivyo mlango
walisahau kuufunga na baada ya kumaliza kupeana zawadi mke alimuuliza
mume "hivi unakumbuka mlango hatukufunga?"
Hii
ni ina maana gani? ni kuthibitissha kwamba muda wote wa tendo la ndoa
mke alikuwa anawaza kwamba mlango haujafungwa na alikuwa anawaza hivi
watoto wakirudi na kuingia moja kwa moja itakuwaje.
Mume yeye wala hakuwa na wazo hilo na wanaume wengi wapo hivyo.
Mwingine ana enjoy sex mwingine anawaza mlango haujafungwa!
Pia sijui inakuwaje tafiti nyingi zinaonesha wanaume wala huwa hawaogopi wapi ni salama kufanya tendo la ndoa.
Kwenye
gari, bafuni, jikoni, sebuleni, chumbani, store, ofisini, kiwanjani,
porini, makaburini na sehemu zingine unazozijua wewe.
Kuna nchi watu walikuwa wanaulizwa maeneo ambayo wamewahi kufanyia sex, ukweli majibu yaliyokuwa yanatoka yanatisha sana.
Tatizo
kubwa lingine ambalo linaweza kuwa kizuizi cha kumpa hamu mke wakati wa
tendo la ndoa ni wanaume kuwa wachafu au rough, au kutozingatia usafi.
Inawezekana
wewe ni mwanaume unafanya kazi ambayo baada ya kazi unakuwa na majasho
au unahitaji kuoga vizuri acha suala la kupiga mswaki na kuwa na kinywa
kisicho na harufu.
Kucha
chafu na mikono inayotisha hata unapomshika bibie na ngozi yake laini
badala ya kusisimuka wewe unamuumiza na kumpa kinyaa kama si
kichefuchefu.
Bahati
mbaya na huko kazini uliona picha au mwanamke mrembo basi homoni nazo
zikafanya kazi basi ummemkumbuka mkeo hivyo kufika nyumbani tu unataka.
Bila
kujali usafi unamrukia mkeo na kwa kuwa anauwezo wa kunusa zaidi kuliko
wewe unafanya a-palalyse kwa kuishiwa hamu kabisa na wewe matokeo yake
na wewe unajisikia upo rejected.
Ukweli usafi ni jambo la msingi mno.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U