Si vizuri kumtamkia maneno mabaya
mwenzi wako mbele za watu.
Mke au mume anahitaji kuheshimiwa,
kupewa asante kuwa appreciated na zaidi kumsifia mbele za watu na sivinginevyo.
Kuongea mambo mazuri kwa mke au mume
wako mbele za watu ni muhimu sana.
Wapo wanaume hutukana wake zao mbele
za watu na wapo wanawake hujibu mbovu waume zao hata mbele za watu au wageni.
Kama kuna kitu amekuudhi kwa nini usisubiri mkaongee chumbani mkiwa wawili?
2. KUTOSIKILIZA MMOJA AKIONGEA.
Hii inajumuisha kuwa na mawazo ya
mbali wakati mume au mke anaongea, yeye anaongea wewe unaendelea kuangalia TV,
Unaendelea kusoma gazeti, unaendelea kusoma kitabu, Unaisikiliza laptop kuliko
mume wako au mke wako.
Pia hii inajumuisha kuwa mbali
kimwili (body language) wakati mwenzako anaongea, wapo wanandoa ambao hata
mwenzake hajamaliza kuongea tayari anadakiwa kwamba najua ulichokuwa unataka
kusema, pia wapo ambao hata ukiuliza swali yupo kimywa, mbaya zaidi ni pale
unapoona na kuhisi mwenzako ana tatizo lakini ukimuuliza anabaki kimya au
anakwambia hakuna tatizo, Inaumiza sana hasa kwa wenzetu wanawake ambao
asilimia kubwa ya wanaishi kwa hisia, na kuumiza hisia zao ni kitendo kibaya
sana, ni vitu vidogo lakini ni muhimu kuliko unavyodhani.
3. KUKOSA MAHABA.
Ukiacha mke wako au mume wako
anahangaika na kutoridhishwa kimapenzi maana yake unachimba shimo ambalo
ukijifukia utatokea jehanam, na kama unaona umepoteza interest na sex fanya
kila njia kupata ushauri na msaada ili urudi kwenye mstari.
Matatizo mengi ya ndoa zinazokufa
huanza kwa ugonjwa wa kutoridhishwa kimahaba na mume au mke.
Kumbuka ndoto za watu wengi kuoana
ni kupata mtu atakayemtosheleza kimapenzi.
4. KUJIONA SAHIHI MARA ZOTE.
Hii inajumuisha wewe kuwa ndo
msemaji na muelimishaji wa mke wako au mume wako, yaani wewe ndo unajua kila
kitu, upo sahihi siku zote, au bila neno lako la mwisho basi information
haijakamilika.
Siku zingine kubali kwamba umekosea
au huna jibu, hakuna mtu anaweza kufurahia kuwa na mtu ambaye siku zote yeye
ndo yupo sahihi labda kama unaishi na mtu mwenye mtindio wa akili.
5. KUTOKUFANYA KILE UNASEMA.
Siku zote Imani bila matendo imekufa
na Imani ni matendo, “Actions do speak louder than words”. Ukisema utafanya
kitu Fulani, fanya.
Wanawake ni viumbe ambao hutunza
sana ahadi tunazowapa, hivyo usiahidi kitu ambacho huwezi kufanya, kwani
mwenzio anaandika kwenye ubongo wake siku akija kukutolea mahesabu ya ahadi
hewa umefanya utaipata fresh, pia na wanaume (si wote) kwa ahadi hewa
hatujambo, tujifunze kufanya kila tunachosema.
Tusitoe ahadi tamu kumbe hewa,
inaumiza sana.
6. UTANI UNAOUMIZA.
Kama mwenzio anakwambia utani wako
unamuumiza achana nao, kuna utani mzuri lakini kuna wakati mnaweza kufikishana
pabaya na lazima uwe makini kusoma saikolojia za mwenzi wako, kuna wengine
anaweza kukutania wewe usikwazike, na utani huohuo ukimrudishia yeye anakwazika
so be very careful usimuumize mwenzako.
7. KUTOKUWA MWAMINIFU.
Kudanganya na kuwa na siri zako
binafsi katika mahusiano huweza kujenga wawili kuwa mbali na kutokuaminiana.
8. KUWA MTU UNAYEUDHI KILA
WAKATI.
Inaweza kuwa ni mzembe, mchafu, mtu
wa kuchelewa kila mahali, mtu wa kusahihisha kila kitu mwenzio anafanya, mtu wa
kulalamika tu kila wakati kila kitu, kuwa kimya tu mwenzio akitaka muongee
masuala ya ndoa au familia. Unajua unaudhi lakini unaendelea kuudhi.
9. KUWA MCHOYO.
Yaani unatumia pesa nyingi sana kwa
mambo yako na mume wako au mke wako akitumia pesa kidogo tu kelele na zogo hadi
nyumba inakuwa moto.
Hadi nyumba yako haipo friendly
maana hata kuburudika kwa soda tu kwako ni issue wakati ukiwa mwenyewe
unajichana ile mbaya na kuku kwa chips na kitimoto na watu ambao ni nje na
familia yako, hiyo ni aibu!
10. UKALI ULIOPITILIZA.
Kila mwanandoa anahitaji kuwa
mstaarabu linapokuja suala la kutatua mgogoro wowote, wapo ambao tatizo
likitokea mke au mume na watoto wanatamani kuhama nyumba maana hapakaliki, Ni
kweli kwa kelele zako na mihasira yako unaweza kuwin huo mgogoro lakini mbele
ya safari bado utajikuta ni wewe ndo umeharibu zaidi.
Sidhani kama kuna mtu anapenda
kukaripiwa kama mbwa ndani ya ndoo.