Watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka matano ya uvunjivu wa sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo vya wanafunzi 32,walimu wawili na dereva mmoja .
Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu,
Desdery Kamugisha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Mwendesha
Mashitaka wa serikali, Rose Sulle aliieleza mahakama hiyo kwamba,
washtakiwa hao walitenda makosa hayo Mei 6, mwaka huu katika eneo la Kwa
Morombo jijini Arusha.
Alieleza kuwa mshitakiwa wa kwanza ambaye ni mmiliki wa shule hiyo anakabiliwa na makosa manne huku shtaka la tano likiwahusu washtakiwa wote wawili.
Aidha Mahakama hiyo imewaachia huru mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Innocent Mosha na Makamu Mkuu Logino Vicenti kwa dhamana ya Sh15m kila mmoja.