Saturday, May 13, 2017

Published 5/13/2017 10:11:00 PM by

WANAUME WABAYA NINYI! Ni miaka miwili tangu niachwe niachwe na mume wangu niliyezaa naye watoto wawili. Cha ajabu mtu aliyechangia kuvunjika kwa ndoa yangu ni mama mkwe, nilimpenda sana mama. Nilimshauri mume wangu achukue mkopo na kumfungulia mama mradi lakini alichokuja kunilipa ni kuniharibia ndoa yangu. Niliumia sana, niliteseka mno, sikuwa naweza kula, kunywa zaidi ya kulia na mawazo mengi. Mwili wangu mzuri niliokuwa nao ulipukutika kabisa na kuwa kama mgonjwa. Naam nilikuwa mgonjwa wa MATESO YA MAPENZI. Nyumbani walijitahidi kufanya kila mbinu ili niweze kurudi katika hali yangu lakini haikuwezekana. Nilipewa makombe lakini nayo hayakusaidia. Nilikata tamaa ya maisha, nilitamani japo nife ili niepukane ma mateso yaliyo mbele yangu. Baada ya mateso nilifanikiwa kuwasiliana na G Wa M&U nikamsimulia kila kitu kwani siku hiyo aliandika makala ambayo nilihisi ameniandikia mimi kwani alichokiandika kilinigusa. Alinishauri kwa siku kadhaa nilianza kurudi kwenye hali yangu ya kawaida, nyumbani wakaanza kushangaa wakahisi labda mume wangu kanirudia lakini haikuwa kweli. Tabasamu usoni pangu lilianza kuonekana kama zamani, nikaanza kula kama zamani, furaha na raha zikaanza kurejea na hata mwili ukaanza kurudi. Namshukuru sana G kwani alinifanya niendelee kuishi, ni zaidi ya ndugu yangu, nyumbani walitaka kumuona na kumpa japo chochote lakini muda wake haukumruhusu kuja kwetu. Nilikubalina na ukweli kuwa nimeachwa, G alinifundisha ujasiri, kukubali ukweli, kuanza maisha mapya bila kumtegemea mwanaume. Nimeishazoea leo mzazi mwenzangu anarudi kwa upole anadai kuwa nirudi kwake kabla Mwezi Mtukufu ili tulee watoto wetu. Nimeumia sana kwa ajili yake nimeteseka bila kumkosea. Kama umesoma waraka huu naomba ushauri wako, niko njia panda mwenziyo ila HAWA WANAUME NI WABAYA NINYI! Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali. Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook. Na:M&U




Ni miaka miwili tangu niachwe niachwe na mume wangu niliyezaa naye watoto wawili.

Cha ajabu mtu aliyechangia kuvunjika kwa ndoa yangu ni mama mkwe, nilimpenda sana mama. Nilimshauri mume wangu achukue mkopo na kumfungulia mama mradi lakini alichokuja kunilipa ni kuniharibia ndoa yangu.

Niliumia sana, niliteseka mno, sikuwa naweza kula, kunywa zaidi ya kulia na mawazo mengi. Mwili wangu mzuri niliokuwa nao ulipukutika kabisa na kuwa kama mgonjwa. Naam nilikuwa mgonjwa wa MATESO YA MAPENZI.

Nyumbani walijitahidi kufanya kila mbinu ili niweze kurudi katika hali yangu lakini haikuwezekana. Nilipewa makombe lakini nayo hayakusaidia.

Nilikata tamaa ya maisha, nilitamani japo nife ili niepukane ma mateso yaliyo mbele yangu. Baada ya mateso nilifanikiwa kuwasiliana na G Wa M&U nikamsimulia kila kitu kwani siku hiyo aliandika makala ambayo nilihisi ameniandikia mimi kwani alichokiandika kilinigusa.

Alinishauri kwa siku kadhaa nilianza kurudi kwenye hali yangu ya kawaida, nyumbani wakaanza kushangaa wakahisi labda mume wangu kanirudia lakini haikuwa kweli.

Tabasamu usoni pangu lilianza kuonekana kama zamani, nikaanza kula kama zamani, furaha na raha zikaanza kurejea na hata mwili ukaanza kurudi.
Namshukuru sana G kwani alinifanya niendelee kuishi, ni zaidi ya ndugu yangu, nyumbani walitaka kumuona na kumpa japo chochote lakini muda wake haukumruhusu kuja kwetu.
Nilikubalina na ukweli kuwa nimeachwa, G alinifundisha ujasiri, kukubali ukweli, kuanza maisha mapya bila kumtegemea mwanaume.

Nimeishazoea leo mzazi mwenzangu anarudi kwa upole anadai kuwa nirudi kwake kabla Mwezi Mtukufu ili tulee watoto wetu. Nimeumia sana kwa ajili yake nimeteseka bila kumkosea.

Kama umesoma waraka huu naomba ushauri wako, niko njia panda mwenziyo ila HAWA WANAUME NI WABAYA NINYI!

Kwa ushauri wa mahusiano, hadithi za mapenzi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali.

Jiunge na M&U WhatsApp na M&U SMS kupitia 0679979785 au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Na:M&U


      edit