Makosa tuliyofanya tukashindwa
kufaulu masomo, au tukafukuzwa kazi, au biashara zetu zikafa. Wakati uliopita
umebeba mengi na ndiyo umekufikisha hapo ulipo sasa. Maamuzi uliyofanya siku
zilizopita huko nyuma, ndiyo yamekufikisha hapo ulipo. Watu uliokuwa karibu nao
siku zilizopita, ndiyo wamekusaidia kujenga maisha uliyonayo sasa. Mawazo
uliyoruhusu yatawale akili yako siku za nyuma, ndiyo yamekaribisha kila
ulichonacho sasa kwenye maisha yako. Kwa kifupi upo hapo ulipo sasa, kwa sababu
ulichagua hivyo siku zilizopita. Najua utabisha kama bado unaamini wazazi wako
ndiyo wamekufikisha hapo, au serikali ndiyo imekufikisha hapo, ila usikate
tamaa, nitakuonesha namna ya kutoka hapo ulipo sasa muda siyo mrefu.
Mbili; wakati uliopo sasa.
Wakati mwingine ambao unao kwenye maisha yako, ni wakati uliopo sasa, wakati huu, hivi unavyosoma hapa sasa, ndiyo wakati ambao unao. Huu ni wakati muhimu sana kwa sababu ndiyo unatengeneza kesho yako. Kama tulivyoona kwenye wakati uliopita, ndiyo umetengeneza wakati uliopo sasa, wakati ulionao sasa ndiyo unatengeneza wakati ujao. Kila unachofanya sasa, hapo ulipo unatengeneza matokeo ya kesho. Namna unavyofanya kazi au biashara yako, ndiyo mbegu unayoipanda kwa ajili ya kesho. Mawazo unayoruhusu yatawale akili yako sasa, ndiyo yanatengeneza kesho yako. Na hata watu wanaokuzunguka sasa, ndiyo wanakusaidia kuijenga kesho yako. Chochote unachofanya sasa, hakitaenda bure, bali kitaijenga kesho yako, iwe ni kitu kizuri au kibaya.
Tatu; wakati ujao.
Huu ni wakati ambao bado hatujaufikia, ni wakati ambao unakuja, na hatuna uhakika utakuwaje wakati huo. Hakuna mtu yeyote amewahi kufanikiwa kutabiri kwa uhakika wa asilimia 100 kwamba wakati unaokuja utakuwaje. Hakuna ambaye amewahi kuiona kesho, lakini tuna matumaini itakuwa bora, na mambo yatakuwa kama sasa au bora zaidi. Wakati ujao ni matumaini kwetu, ndiyo unaotusukuma tuweke juhudi zaidi leo, ili wakati huo uwe bora sana. Ndiyo maana tunakazana kuwekeza, kuweka akiba na mengine ili kuhakikisha kesho, kwa vyovyote itakavyokuja, basi tutaendelea kuwa vizuri. Kesho inatusukuma kuchukua hatua leo, ili inapokuja, tusiwe kwenye wakati mgumu.

Tatizo kubwa tunaanza kulitengeneza hivi.
Sasa lipo tatizo kubwa sana kwenye hizi nyakati tatu, tumekuwa hatuziishi kama ambavyo tumezielezea hapo juu, kwamba nyakati zilizopita ni jana, wakati uliopo ni leo na wakati ujao ni kesho. Badala yake tumekuwa tunavuruga kila wakati na mbaya zaidi kujinyima wakati wa kuishi ni sasa.
Picha huwa linaanza pale tunapofikiria wakati uliopita, makosa ambayo tumefanya, fursa ambazo tumezikosa, na kujiona kama tumepoteza sana. Tunajilaumu kwa nini tulifanya au hatukufanya kitu fulani. Tunajitesa kwa makosa tuliyoyafanya huko nyuma. Na yote haya, tunayafanya kwenye wakati tulionao sasa, ambao tulipaswa kufanya mambo ya sasa.
Hatuishii hapo, bali tunaiangalia na kesho pia, wakati ujao. Tunaangalia wakati huo kwa hofu kubwa, tukiona mambo yatazidi kuwa mabaya, hali itazidi kuharibika, maisha yatazidi kuwa magumu na hatutaweza tena kupiga hatua. Tunajenga picha moja mbaya na ya hatari sana, picha inayotufanya tushindwe kabisa kupiga hatua yoyote ile, na kubaki kama tumepingwa sindano ya ganzi. Hili linachangia zaidi kuharibu wakati tuliopo sasa.
Kwa kuchanganya yale tuliyofanya au kutokufanya wakati uliopita, na kufikiria mabaya zaidi kwa wakati ujao, tunajikuta hata wakati tulionao sasa hatufanyi chochote. Hatuchukui hatua yoyote ambayo ingeweza kubadili hali ya mambo hapo kesho, badala yake tunajaza akili yetu mawazo ambayo hayawezi kutusaidia. Mawazo ambayo yanatupa hofu zaidi ya kufanya, na tunabaki hatujui tufanye nini. Hapa ndipo wengi hukata tamaa na hata wengine kufikia kukatisha uhai wao.
Ipo njia ya kuhakikisha kesho yako inakuwa na mafanikio makubwa.
Na njia hiyo siyo ngumu kama unavyofikiri, bali ni rahisi sana, na ni kuchagua kuishi leo.
Kwenye njia hii, unachagua kuishi leo, kwa sababu kile unachofanya leo ndiyo kinaandaa kesho yako. Kwa njia hii unatambua yale yaliyopita, lakini unakubali kwamba haijalishi utafanya nini, huwezi kubadili chochote ambacho kimepita, huwezi kurudi na kufuta makosa yaliyopelekea kufeli, kufukuzwa kazi au biashara kufa. Huwezi kurudi nyuma na kuzichukua zile fursa ambazo zilikupita. Lakini unajua kwamba kwa kufanya kitu leo, kwa kuchukua hatua leo, basi unaitengeneza kesho yako vizuri zaidi. Unachofanya kwa wakati uliopita ni kujifunza na kusonga mbele.
Pia kwa wakati ujao, ambao tumekuwa tunautengenezea hofu, tunakubali kwamba hatuwezi kuujua kwa uhakika, na hatuwezi kuuishi kabla haujafika. Hivyo kupoteza muda mwingi kuufikiria kwa hofu, hakutatusaidia lolote kwa sasa. Hivyo tunautumia kama hamasa ya sisi kufanya kitu leo.
Kazi kubwa kwetu ni kuishi kwenye wakati tuliopo sasa, kuchukua hatua kwenye wakati huu, kufanya kitu sasa. Kuyaangalia kwa kina mawazo ambayo tumeruhusu yatawale akili yetu sasa, je ni mawazo yanayotujenga au kutubomoa? Ni mawazo chanya au hasi? Pia tuangalie wale ambao wanatuzunguka, je kuna mahali popote wanaenda na maisha yao au wapo wapo tu. Ni watu ambao wana msaada kwetu au wanaturudisha nyuma? Ni muhimu pia kuangalia kila jambo unalofanya sasa, kila hatua unayopiga sasa na kuona kama ina mchango wowote kwenye kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi leo na siku zijazo.
Namna unavyofanya kazi yako na hata biashara yako, je inaongeza ufanisi zaidi?
Unatengeneza thamani zaidi?
Ili kuishi vizuri leo, na kuweza kuitengeneza kesho ambayo ni bora zaidi, basi zingatia yafuatayo;
1. Kuwa na maono makubwa ya siku zijazo, mwaka mmoja kutoka sasa, miaka mitano, miaka kumi na kuendelea. Siyo lazima uyafikie kama yalivyo, lakini yatakusukuma kuchukua hatua.
2. Hakikisha kuna hatua unachukua leo, ambayo itakufanya kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa jana.
3. Usikubali kuzungukwa na watu ambao hawajui wapi wanakwenda, kaa mbali na watu hasi.
4. Usipoteze muda wako kujutia makosa uliyofanya huko nyuma, au fursa ambazo hukuzichukua.
5. Tumia muda wako wa leo vizuri, usipoteze hata dakika moja, poteza fedha utazipata nyingine, poteza muda na hautaupata tena.
Fanya haya rafiki, na kesho yako, kwa hakika haitakuwa kama ilivyo leo, au ilivyokuwa jana. Japo huwezi kujua kwa hakika itakuwaje, lakini itakuwa bora zaidi.
BY Tatu Kiondo