Mafanikio siku zote
yanakuja kutokana na wewe kujenga uwezo au nguvu ya kukusaidia kufanikiwa kila
siku. Hapo nikiwa na maana ni muhimu kujua kila siku, unatakiwa kutengeneza
nguvu fulani ya kukusaidia kufanikiwa hata katika kipindi ambacho unajiona kama
vile umechoka.
Bila kutengeneza nguvu
kubwa ya kuweza kukusaidia kufanikiwa moja kwa moja, uwe na uhakika kuna wakati
utakwama kufika kule unakotaka kufika. Pengine unajiuliza nguvu hii utaipataje
ya kukusaidia kufanikiwa ili na wewe uweze kuitumia na ikusaidie?
1.
Tafuta nguvu yako kubwa inapatikana muda upi.
Ni rahisi sana kujenga
nguvu ya kukusaidia kufanikiwa katika maisha yako kila siku, ikiwa utajua nguvu
hiyo kubwa ya kukusaidia kufanikiwa
inapatikana muda upi. Ni lazima ujue nguvu hiyo unaipata asubuhi, mchana au
jioni?
Kwa wengi ili waweze kufanya
mambo kwa kishindo na mafanikio makubwa, masaa yao ya mwanzo ya asubuhi
huyatumia sana kufanya vitu ambavyo vinawapa faida na mafanikio kwao kwanza.
Ni masaa ambayo hawana mchezo
nayo. Ni masaa ambayo siyo wanayatumia kwenye mitandao ya kijamii. Ni masaa
ambayo yametengwa binafsi kwa ajili yao.
Kwa nini hiyo iko hivyo?
Ni kwa sababu asubuhi mara nyingi ni muda ambao unakuwa umetulia sana, hivyo ni
rahisi kufanya mambo mengi wakati akili ina nguvu nyingi ya kukusaidia kukupeleka
kwenye mafanikio.
Hata wewe ili uweze kutengeneza
nguvu kubwa itakayokusaidia moja kwa moja kufanikiwa unalazimika kutafuta muda
wako bora wa kukufanikisha. Kumbuka, nguvu yako kubwa ya mafanikio inapatikana kwa
kujua ipo muda upi. Ukilijua hilo fanyia kazi.
2.
Anza na kidogo ulichonacho.
Ili upate nguvu kubwa
itakayokusukuma kuweza kufikia mafanikio makubwa, unalazimika kuanza na kidogo.
Kama ni biashara anza na mtaji wowote ulionao halafu baadae mtaji huo utauwa
ukiongezeka siku hadi siku.
Kwa chochote kile unachoanza
nacho hata kama ni kidogo sana ukikifanya kwa muda mrefu kinakuwa kikubwa na
kinakupa nguvu kubwa ya kuweza kukusaidia kufanikiwa moja kwa moja.
Kipi kidogo ulichonacho
unashindwa kuanza nacho? Kuanza na kidogo ulichonacho ni moja ya kanuni kubwa
sana ya kimafanikio ambayo unaweza kuitumia na kukutengenezea nguvu kubwa ya
kimafanikio kwako.
3.
Jenga nidhamu kubwa sana.
Kama kweli umeamua
kutengeneza nguvu kubwa ya kukusaidia kufanikiwa, nidhamu ni muhimu sana.
haijalishi unakutana na nini au dunia imegeuka chini juu, lazima ujenge
nidhamu.
Katika kile kidogo
ulichoanza nacho, ukikijengea nidhamu ya muda mrefu, utashangaa maisha yakibadilika
na ukizidi kusogea kwenda mbele kimafanikio kuliko vile unavyofikiri.
Nidhamu ni msingi mkubwa sana
wamafanikio makubwa na pia inakujengea nguvu kubwa ya kukusaidia kufanikiwa
moja kwa moja hata kama kuna watu walikuita hujiwezi au umechoka.
4.
Weka pembeni tabia zinazokukwamisha.
Sina shaka kabisa upo hapo
ulipo kimaisha kwa sababau tu ya yatabia fulani fulani ambazo umezishikilia kwa
muda mrefu na zimekufikisha hapo ulipo. Sasa ili ufanikiwe ziweke pembeni tabia
hizo.
Hutaweza kutengeneza nguvu
kubwa ya kukusaidia kufanikiwa kama kweli bado unaendelea kushikilia tabia
fulani fulani hivi zinazokuzuia kufanikiwa moja kwa moja kwenye maisha yako.
Kama ni uvivu, uweke
pembeni, kama ni kupoteza muda weka pembeni, kama kutokujifunza weka pembemni,
kisha amua sasa kuchukua tabia zile zitakazo kusaidia kuweza kujenga nguvu ya
kufanikiwa moja kwa moja.