Msanii wa muziki wa hip hop, Nikki wa Pili amefafanua kauli yake ya
uchunguzi ufanyike katika ajali iliyoua 32 Arusha baada ya kudai kuna
baadhi ya watu wameshindwa kuielewa kauli yake hiyo.
Rapa huyo amedai kuwa ni jambo la utu
kama tatizo litajulikana na kufanyiwa marekebisho kwa vitendo na siyo
kuhukumu watu au kumtafuta mchawi nani kipindi hiki, huku akitaka
asinukuliwe vibaya.
“Nasikitika watu wameninukuu vibaya sana
niliposema uchunguzi ufanyike wengine wameniponda lakini sijachukia
kwani hawajanielewa “Uchunguzi ukifanyika sina maana ya kumhukumu mtu mmoja hapana
bali tuweze kujifunza. Watu wengi waliokusanyika uwanjani kuaga walimu
na wanafunzi wameonyesha utu lakini pasipo tukio hili kuchunguzwa utu
wao utakua hauna thaani kwani matatizo haya yatajirudia mara kwa mara,”
Aliongeza, “Inawezekana kuwa mikanda
ilikosekana kwenye ‘bus’ walilokuwa wamepanda wanafunzi na walimu wa
Lucky Vicent Academy au mwendo haukuwa mzuri lakini tatizo linaweza kuwa
hali ya hewa hivi ni vitu ambavyo vikifanyiwa uchunguzi vinaweza
kutukumbusha tabia zetu na tutajifunza wakati mwingine,”
Katika hatua nyingine Nikki amewaona watu
wanaoweka mitandaoni picha za ajali na kusema kuwa ni vitendo
vya udhalilishaji na kuongeza kwamba zipo njia nyingi za kutoa taarifa
kwenye mitandao lakini siyo kwa ku- ‘share’ picha za ajali ambazo watu
wanakuwa wameumia vibaya.
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza HapaNa.M&U