Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kila jambo katika maisha yangu ya kila siku, najua yapo mengi sana ambayo namkosea. Kwa maneno, matendo na hata kwa kushindwa kutimiza wajibu.
Lakini kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema bado naipa nafasi ya kuweza kuzungumza na wewe. Tutende mema ndugu zangu. Nikukaribishe kwenye somo la ujasiriamali linalosema:KWA NINI UKATISHWE TAMAA NA MWENYE KUKATA TAMAA!
Ugumu wa maisha anao kila mtu kulinga na uzito wake, kuna wengine wana hali ngumu zaidi lakini kuna wale wenye ahueni.
Katika mafanikio yoyote yale yana changamoto nyingi zipo za mazingira, mtaji, ushauri au watu wanaokuzunguka.
MAZINGIRA
Maeneo uliyopo yanaweza kuwa kigezo cha kukukatisha tamaa kwa namna moja au nyingine katika kufikia jambo fulani. Mazingira unayoishi ni magumu kufanya kile unachokita. Inawezekana umejaribu kila namna lakini bado ikashindikana basi ni vyema ukahama hilo eneo la kwenda eneo ambalo unahisi litakuwa mafanikio kwa kile unachokitaka. Angalizo wakati mwingine ni vyema ukatafuta fursa kulingana na eneo lako.
WATU
Wapo watu wengine wana maono au ndoto nzuri lakini zinashindwa kufanikiwa kwa sababu wanakatishwa tamaa na watu ambao walishakata tamaa zamani kwenye mioyo yao.
Watu wanaoweza kukukatisha tamaa anaweza kuwa ndugu, rafiki au mpenzi wako. Ni vyema wakati unataka ushauri ukachagua mtu au watu wa kukushauri kuliko kuomba ushauri kwa mtu yeyote.
MPENZI
Inawezekana una mpenzi ambaye anakukatisha tamaa kwa sababu wewe una tatizo fulani katika mwili wako labda pengine una ulemavu wa kitu fulani, huna elimu, huna pesa, huna kitu chochote cha maana.
Usikubali kumpa nafasi mtu ambaye ameishakata tamaa siku nyingi, mtu ambaye ana amini kuwa mafanikio yako kwa baadhi ya watu.
Hupaswi kukatishwa tamaa na mwanadamu ambaye ana mapungufu kama wewe, anaumwa kama wewe, analala kama wewe, anahangaika kama wewe, anaugua kama wewe, anakata tamaa kama wewe, alifeli masomo kama wewe, hana kitu kama wewe, siku moja atakufa kama wewe.
Binadamu wengine unaweza kusema labda wamezaliwa kuja kuwamatisha tamaa wenzao yani kila jambo ukifanya umekosea, kila kitu ukisema ni kibaya, wewe mtu wa aina gani, hakuna jema kwako.
Mtu wa namna hiyo ni yule ambaye amefeli katika kufikiria, upeo wake umegota sehemu aamini kama unaweza kuleta maajabu kwa umaskini ulio nao, kwa elimu ndoto uliyonayo, kwa ushamba ulionao. Pigania ndoto zako, acha kusikiliza maneno ya watu ukitaka kuamini kuwa hawafai, wewe acha kutimiza ndoto zako usikie watakavyokusimanga lakini hakikisha umefikia uone kama hawajakusifia kiaina.
Ushauri wangu kwa wapenzi ni vyema mkawa mnashirikishana katika kutimiza ndoto zenu hiii itasaidia inawezekana wewe mpenzi au mkeo unamuona bogaz nyumbani lakini ofisini kwake ni kichwa ni mwanamke ambaye anategemewa katika maamuzi ya kampuni, mtumie na nyumbani ili muanzishe kampuni yenu.
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U