Monday, December 26, 2016

Published 12/26/2016 09:05:00 AM by with 0 comment

ACHA KUDANGANYWA NA PENZI LA MSIMU!

Asante Mungu kwa kunisimamia na kuimaliza siku hii vizuri, ni kweli sijafanikiwa kunua nguo mpya, kiatu, chakula kipya, kwenda kiwanja wa sijafanikiwa kunywa kinywaji au kilevi kwa sababi leo ni sikukuu.

Ila nimefanikiwa kuimaliza siku salama nikiwa sina jeraha, sina kovu, sijalazwa hospitalini, sijafikishwa polisi na wala sijapoteza uhai wangu na ndiyo maana nimeandika makala haya.

Kama wewe umekuwa ukioneshwa upendo au penzi la msimu basi hii inakuhusu sana.

Haiwezekani mpenzi wako ambaye alikuwa amekuchunia kwa muda mrefu leo hii kaona msimu wa sikukuu ndiyo anajifanya anakupenda, ana kumisi, huo ni uongo, ni utapeli.

Mpenzi wa namna hiyo ni kuwa naye makini sana, si ajabu amekosa sehemu ya kushika katika kipindi hiki cha sikukuu, kwani kila akigusa pamenuna, kila akifanya hivi haoni pa kushika hivyo kakumbuka kuwa wewe ni mmoja wa watu ambaye unampenda sana na ndiyo maana katumia fursa hiyo kujisongeza mzimamzima hasa kipindi hiki cha sikukuu.

Anajua madhaifu yako ndiyo maana kajisogeza, anajua huna ubavu kwake ndiyo maana kajifanya kuwa bado anakupenda ili akulie vyako, ndugu yangu maji huwa hayasahau baridi hata yachemshweje, stuka unaliwa!

Mpenzi wa kweli mwenye penzi la dhati, anakupenda na kukujali muda na siku yoyote bila kujali kama ana pesa au hana.

Lakini siyo anayekujali pindi ambapo anakuwa na kitu, inaonesha mpenzi wa namna hiyo hana utu, anajua wewe bila pesa huendi ni sawa na punda bila mjeredi.

Mapenzi matamu ni yale yakusaidiana, kupendana kujuliana hali muda wote haijalishi umbali mlioko.

Poleni sana ambao mmeingizwa choo cha watoto na kutapeliwa na wapenzi wenu katika msimu huu wa sikukuu.

Poleni nyote ambao mmeimaliza sikukuku kwa kudundwa mangumi kwa sababu ya mambo ya kijinga, pole sana uliyekosana na mapenzi, mchumba au mume wako kisa kikiwa ni mchepuko.

Jiangalie, kama mchepuko wako anakupenda kuliko mumeo si akuweke ndani, ila kwa kuwa hawezi, hakupendi ndiyo maana kakugombanisha na mtu anayelisha, anayekuvisha, anayekuweka mjini baada ya kukutoa huko maporini.

Mapenzi ya msimu ni mabaya sana, yanakufanya ujiaminishwe kuwa unapendwa kumbe hakuna chochote zaidi ya kutumika kimapenzi.

Kwa leo yangu ni hayo, tu, kwa kuwa wewe ni kichwa maji yataingia sikio moja yanatokea jingine.

Nikutakie usiku mwema, tukutane tena kesho. Kwenye MKASA WA KWELI WA "NIMEAMUA KUJIUZA."

Unaweza kupata mikasa, mada za mahaba, ushauri wa mapenzi na ujasiriamali kupitia  M&U SMS za kawaida na M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimia na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.

      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.