Saturday, December 17, 2016

Published 12/17/2016 07:32:00 AM by

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU UKIMWI

Moja ya changamoto tulizonazo katika mapambano dhidi ya VVU ni tatizo hilo kugusa kila rika na zaidi hasa vijana ambao wako katika hatari ya kupata maambukizi. Ingawa ugonjwa huu umedumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa, lakini bado kuna maswali mengi ambayo watu hawayafahamu kuhusu ugonjwa huu.

Nimeona nitumie nafasi hii kujibu maswali ambayo wengi wamekuwa wakiniuliza hasa baada ya kuanza kuleta makala zinazozungumzia VVU.

Nimechambua maswali ambayo nikiyajibu nadhani yatakuwa na tija katika ufahamu wa elimu ya VVU na sitataja jina la mtu aliyeuliza.

Swali: Mimi ni mjamzito, je kama nimeambukizwa VVU mtoto aliye tumboni anapataje VVU?na je kama anapata kuna njia ya kuweza kusaidia nijifungue bila VVU?

Jibu: Mtoto anaweza kupata VVU akiwa tumboni, wakati wa kujifungua na wakati wakunyonyesha. Jibu la pili njia yakuzuia maambukiz ya mama kwenda kwa mtoto ipo na jambo la msingi ni kuhudhuria kliniki ya mimba mapema kwa ajili ya ushauri na upimaji, kama ukigundulika hatua za haraka huchukuliwa kabla ya kujifungua na utapewa dawa maalumu.

Swali: Je kama nimejamiiana na mtu mwenye VVU na nikaambukizwa je, naweza kupima na kupata majibu siku hiyo hiyo niliyojamiiana?

Jibu: Kuna kipindi kinachoitwa kipindi cha mpito, VVU kuweza kuzaliana na kuweza kugundulika ambacho huwa ni baada ya miezi 3, vipimo vikubwa kama vile PCR na ELISA huweza kugundua maambukizi kwa mda wa siku 7-14 na vipimo vya haraka vinavyotumika hapa mara nyngi ni determine na bioline ambacho huweza kugundua maambukizi katika damu baada ya siku tatu toka siku ya kwanza ya maambukizi.

Swali: Je, ni kweli kuna aina mbili za VVU? Kama ndivyo hapa nchini kwetu ipi ina idadi kubwa ya kuambukiza?

Jibu: Ni kweli zipo aina mbili za HIV-1 na HIV-2. Hapa nchini na Afrika Mashariki ni HIV-1 ndiyo ina wagonjwa wengi zaidi ya 90% na huwa haina makali. HIV-2 inapatakina Afrika Magharibi na huwa ni hatari sana kwani mgonjwa humchukua muda hata wa mwezi kuumwa sana na kupoteza maisha kwa haraka.

Swali: Ni kwa nini watu wengine wana VVU lakini hawapati Ukimwi?

Jibu: Virusi Vya Ukimwi ni Ukimwi.Upungufu wa Kinga Mwilini, hutokea baada ya chembe hai za mwilini (kinga ya mwili) kushambuliwa na VVU.

Kwa kawaida VVU wakiingia mwilini huzivamia chembe hai nyeupe ambazo ndio walinzi wetu wakuu, chembe hizi huwa na vipokezi maalumu (receptor) vinavyoendana na virusi. Mtindo huu ni kama vile virusi ni ufunguo na vipokezi hivi ni vitasa. Sasa baadhi ya watu hawapati Ukimwi kwa kuwa hawana vipokezi hivi au wanavyo ila havimpi kirusi uwezo wakujipachika. Tafiti zingine zinaonyesha kuwa na aina fulani ya protini katika vipokezi vinavyomnyima kirusi nafasi ya kujipachika na kuingia katika seli nyeupe.

Swali: Je mashine za kunyolea saluni zinaambukiza VVU?

Jibu: Ili uweze kupata maambukizi unahitaji kugusana na majimaji ya mwilini au damu ya mtu mwenye VVU kupitia katika michubuko, hivyo basi kama hili litatokea uwezekano upo. Kwa upande wawatengenezaji wamechukua tahadhari katika hili, mashine kutosababisha michubuko, pia kuviosha vifaa hivyo kwa joto na kemikali kabla ya kutumia mwingine huchangia kupunguza maambukizi.

Maambukizi ya VVU kwa mashine za kunyolea ni 2% ya maambukizi yote.

Swali: Je, kunawa na sabuni baada ya kujaamiiana na mwanamke mwenye VVU kunaua VVU?

Jibu: Zipo baadhi ya sabuni zina kemikali ziitwazo detergent hiki ni kiambata kinachoweza kumlaza (bactericidal) kirusi au kimelea mwingine, hivyo ipo nafasi ya kupunguza uambukizi ingawa ni ndogo sana.

Swali: Je kunyonyana ulimi au kula mate kunaweza kuambukiza VVU?

Jibu: Njia ya mdomo inaweza kuchangia mtu kupata VVU kama mtu atakutana na mtu mwenye VVU mwenye vidonda au michubuko mdomoni nawe pia ukawa una michubuko au vidonda mdomoni, ili kuweza kupata VVU kwa njia ya mate inabidi kulamba mate lita 2 jambo ambalo ni gumu.

Swali : Je ni kweli kila anaegua TB ana VVU?

Jibu: Si wote ila wengi wenye kuugua TB wana VVU, huu ni ugonjwa unaotokana na mfumo wa hewa na huwa haujitokezi kwakuwa kinga yamwili huvizingira, na huweza kumpata mtu akishi navyo mda mrefu bila dalili kujitokeza, pale mtu anapokuwa na VVU kinga ya mwili hushambuliwa na kushuka nakuwa chini, hapo ndipo vijidudu vya TB hupata nafasi ya kujitokeza na dalili huanza, Inakadiriwa duniani kuna wagonjwa wa VVU wenye TB.

Swali: Ni kweli mtu asiyetahiriwa hupatwa VVU kwa urahisi?

Jibu: Ni kweli mtu asiyetahiriwa ana asilimia 60 zaidi ya kupata VVU kulinganishwa na mtu aliyetahiriwa.Hii ni kwa sababu katika ngozi ile ya mbele”govi”kuna vipokea virusi vya ukimwi”HIV receiptors”hii humweka mtu asiyetahiriwa kuwa katika hatari zaidi ya yule aliyetahiriwa. Ndiyo maana pana kampeni ya kitaifa ya “dondosha mkono wa sweta”

Swali: Vipi kuhusu vifaa vya kung’olea meno vinachangia maambukizi ya VVU? Maana huwa havitupwi alivyotumia mwenzako kesho na wewe hivyo hivyo.

Jibu: Ukimwi huambukizwa kwa kugusana kupitia michubuko ya mwili njia ya majimaji ya mwilini au damu ya mtu mwenye VVU, vifaa vya kung’olea meno hutumika na kisha husafishwa na kemikali na katika majiko maalum ya umeme yenye moto mkali unaweza kuangamiza vimelea vya maradhi ikiwamo VVU, kama itatokea taratibu za kiafya za usafishaji wa vyombo hivyo hazikufuatwa na vikatumika kwa mtu mwenye VVU maambukizi kwenda kwa mwingine huweza kujitokeza.

Ni vyema kuepuka kung’olea meno vichochoroni na vituo vya afya visivyotambuliwa na Wizara ya Afya.

Swali: Kama jana nilijamiiana na mtu mwenye VVU naweza kupewa dawa za kuzuia nisipate maambukizi?

Jibu: Huduma hizi zipo tu kwa ajili ya wahudumu wa afya waliojijeruhi na kugusana na damu au majimaji ya mgonjwa mwenye VVU, hupewa huduma maalum itwayo PEP ambayo inahusisha upewaji wa dawa zinazozuia kuzaliana kwa VVU.Matibabu haya hayatolewi kwa watu wa kawaida.

Swali: Je, dawa za ARVs zina athari na unywaji wa pombe?

Jibu: Ndiyo, zina mwingiliano na pombe, lakini kutokana na hatua zilizopigwa na wataalamu wa afya, zipo dawa za ARVs ambazo unakunywa kidonge kimoja wakati wa usiku tu, hivyo inakupa nafasi ya kuweza kunywa pombe. Ingawa bado pombe ina madhara kwa mtu na ukizingatia unaugua ugonjwa ambao unahitaji uimarishaji wa afya.

Swali: Je ni kipimo kipi sahihi kinachothibitisha maambukizi ya VVU maana tumeskia kuna feki?

Jibu: Katika upimaji wa VVU zipo hatua mbili ya kwanza huwa ni kipimo cha huwa ni cha kuangalia uwepo wa askari mwili wanaopambana na VVU (antibody) hupimwa mara ya kwanza halafu hurudiwa baada ya miezi mitatu, baada ya hapo hufuatiwa na kipimo cha pili cha kuthibitisha VVU cha ELISA




Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
 
      edit