Mapenzi ni safari ndefu na ngumu sana, kama haujainza unakuwa unatamani uianze lakini ukishaianza kuna wakati unatamani uigaili lakini huwezi kugaili kwa sababu ya vizingiti na mipaka iliyopo katika ndoa mliyofunga.
Ndiyo maana kuna wengine wanasema ndoa ni ndoano. Mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa takribani miezi miwili, lakini nilipofika kwangu, wiki ya kwanza tulipokutana faragha na mwenzangu wiki iliyofuatia akasema hajisikii kufanya mapenzi na mimi.
Nikavumilia lakini leo hii ni wiki ya pili anasema hivyo, je, ni kweli hasikii hamu ya kufanya mapenzi na mimi? Kama ndiyo nini chanzo, na nifanyeje kurudisha hisia zake ili tuendelee kula raha ya ndoa?
Karibu kwa maoni yako, kwa ushauri wa mahusiano, makala za mahaba, mikasa ya kweli ya mapenzi, hadithi, machombezo na ujasiriamali.
Jiunge na M&U WhatsApp au M&U SMS kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspo