Friday, December 16, 2016

Published 12/16/2016 02:27:00 PM by

USHAURI WAKO: MUME WANGU ANALALA NA MIMI KAMA DADA YAKE!





Habari yako! Mimi ni mwanamke wa miaka 37 nina watoto wawili ambao nimezaa na mume wangu. Kutokana na imani zetu kuwa ni tofauti tulifunga ndoa ya bomani takribani miaika 20 iliyopita.
Watoto wetu ni wakubwa kwa sasa, mmoja yuko sekondari mwingine shule ya msingi, mimi na mume wangu huwa hatuishi sehemu moja kila mtu anaishi mkoa tofauti na mwenzake.

Baada ya likizo ya mwezi Desemba kuanza niliamua kumtembelea mume wangu nikiwa na watoto wetu. Yaliyonikuta hadi nikaamua kuomba ushauri ni kutokana na kuishi mbali na mume wangu kwa zaidi ya mwaka lakini cha ajabu leo ni siku ya pili tuna lala kama kaka na dada yake, hajanigusa wala hatikisiki kwa chochote.

Siku ya kwanza kaja na dawa ya maralia na kudai kuwa anaumwa lakini kilichonishangaza asubuhi nimeamka na kukuta hakuna hata dawa moja aliyomeza.
Nilipochoka zaidi ni siku ya pili ambapo akaanza kujisemesha eti kuwa ngiri imemshika.
Kweli mumeo anaweza kukufanyia hivi, naombeni ushauri wenu hata sijui nifanyaje?

Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

      edit