Saturday, December 24, 2016

Published 12/24/2016 02:00:00 AM by

KAMA KUNA MAKOSA NILIKOSA, NISAMEHE MPENZI WANGU!







Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya na pumzi ya kuuona mwaka mpya wa 2017. Niwape pole wale wote waliofika wakiwa ni wagonjwa, waliofiwa, waliofungwa jela na wenye matatizo mengine. Huna budi kukata taama pamoja na magumu yote unayoyapitia, zidi kumuomba Mola hakika atakusaidia.
Mada ya leo inazungumzia kukiri na kuomba msamaha kama kuna kosa ulilomkosea mwenza wako ili akusamehe. Mwaka mpya ndiyo haswa umeanza na leo ni siku ya pili ya mwaka 2017, ni mwaka mchanga, mwaka ambao ukijipanga vilivyo unaweza kufanya vizuri zaidi.

Mume au mke wangu ninaomba msamaha kama kuna jambo ambalo nilikukwaza, nahitaji kuuanza mwaka mpya nikiwa msafi, nikiwa sina chembechembe za ugomvi na wewe, hata kama nilikukwaza vipi ninaomba msamaha, nimejifunza mambo mengi katika maisha, nikagundua wewe ndiye mume au mke wa maisha yangu, haijalishi magumu na changamoto zote ninazopitia lakini bado nakupenda.
 Umeniumiza vyakutosha ila nimekusamehe nianza mwaka mpya vizuri, najua ulihisi ni sahihi kunisaliti lakini mwisho wa siku umejigundua na kuona wewe ndiye mwenye makosa.


Yapo mambo mengi ambayo nimekukwaza na hata wewe kunikwaza, nadhani ni muda muafaka wa kuachana nayo na kuanza maisha mengine mapya. Tafadhali mpenzi wangu rudisha upendo wako wa zamani kwangu, ninaombe unionesha yale mapenzi uliyonionesha wakati tunakutana.

Ninakumbuka mambo mengi sana ambayo ulinifanyia kipindi kile cha mwanzoni, ulinipenda sana ulinibusu, uliniheshimu, ulinijali na kunilinda, ulikuwa tayari kunipigania na kunitete pale ambao uliona kuna adui katikati yetu lakini leo hufanyi hivyo, inakuwa kama tuliona ili kutimiza lengo tu kuwa umeoa au umeolewa na Fulani.
Kumbuka namna ambavyo ulifurahia kuongozana na mimi kila sehemu lakini sasa hivi hutaki, hauko tayari kana kwamba tuliona kimakosa, mpenzi wangu tafadhali naomba mwaka ujao tuuanze upya, niheshimu kama mumeo au mkeo.

 Unaweza kupata mikasa huu kwa kujiunga na M&U SMS kila siku kupitia Na.0657486745.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
MKASA WA NIMEMUA KUJIUZA UTAKUPOSTIWA KILA SIKU KUANZIA SAA 9 ALASIRI

Na.M&U
      edit