Nashukuru Mungu kwa kunipa mume mwema ila ni kweli nimeamini kila binadamu ana madhaifu yake kwani mume wangu pamoja na wema wake alionao lakini hapendi niende kusalimiwa kwetu.
Nimejaribu kukaa naye na kumuelewesha lakini ninaona bado anakuwa mgumu sana kwenye hilo. Kila nikimwambia kuwa nahitaji kusafiri kwa ajili ya kwenda kuwasalimia ndugu zangu anageuka mbogo.
Pamoja na kugeuka huko mboga pia ndani hakukaliki hata zaidi ya siku mbili atakuwa analizungumzia suala hilo na kusafiri. Cha ajabu yeye anasafiri na nikimwambia mbona yeye huwa anasafiri? Ananiambia yeye ni mwanaume na ni baba mwenye nyumba sipaswi kushindana naye.
Ninaumia sana kwani naona kama amenioa ili kunitenganisha na ndugu zangu, haiwezekani nisiende kuwasalimia japo wiki moja!.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U