Friday, December 23, 2016

Published 12/23/2016 03:00:00 PM by

FANYA HIVI MWAKA 2017 KUFIKIA MALENGO YAKO-1





SOMO la leo lina lengo la kukuhimiza kujitahidi kufikia ndoto zako bila kujali umefeli mara ngapi, umeachwa mara ngapi, umeumizwa au kupigwa mara nyingi, yote hayo yachukulie kama changamoto katika maisha yako, lakini kwa mwaka mpya wa 2017, haijalishi kama hukufanikiwa au la, kikubwa ni kujipanga kwa kufanya mambo yale yale lakini kwa mbinu mpya.

Watu wengi wamekuwa wakitamani tu kupata pesa nyingi kwa haraka bila ya kuwa na mipangilio madhubuti katika kuzitafuta au kutengeneza njia za kuzipata pesa hizo. Kama wewe ni miongoni mwao basi badilika kupitia makala hii.

Kila mtu ana ndoto au malengo yake katika maisha, bila kujali ukubwa wa ndoto au malengo kwani yanatofautiana kutoka kwa mtu mmoja na mwingine. Na ndoto hizo hakuna anayeweza kukufanya uzifikie isipokuwa ni wewe mwenyewe kwa msaada wa watu wanaokuzunguka.

Lakini kama utakaa na wazo lako ukisubiri mtu aje akusaidie ni sawa na kufa bila kelele, kufa huku unajiona bila kujitetea, jambo ambalo kwa mtu mwenye uchungu na ndoto, hayuko tayari kuvumilia misemo hiyo.

Kama umeharibu mwaka 2016 basi mwaka ujao unavyaoanza jipange mapema zaidi, anza kwa kujiuliza kwa nini mwaka huu umefeli au umeshindwa kufikia malengo au ndoto zako.

Orodhesha vitu vyote ambavyo vimesababisha ili mwaka ujao utakapoanza kupigania ndoto zako uwe unafahamu namna ya kukabiliana na zile changamoto ambazo zilikukwambisha mwaka huu.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia unaweza kupata mikasa huu kwa kujiunga na M&U SMS kila siku kupitia Na.0657486745.
Unaweza tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa


Na.M&U
      edit