Thursday, December 22, 2016

Published 12/22/2016 02:00:00 PM by

MKASA WA KWELI: NIMEAMUA KUJIUZA!-4



Nilipoishia…
Nikiwa nimeishaanza kukata tamaa na kuhisi labda pengine mchumba wangu Maiko atakuwa kwenye matatizo, ghafla nikaona amepokea, ila nikastaajabu akiniuliza swali ambali sikulitegema kulisikia kutoka katika kinywa chaka hasa ukizingatia tulikuwa na muda mrefu hatujawasilia.

Endelea nami…

“Unasemaje” sauti ya Maiko ilisikika upande wa pili ikiongea kwa jazba, jambo ambalo sikuamini, kwani nilizoea kumsikia Maiko akiwa katika sauti nzuri, ya upendo na furaha.

Ghafla tumbo lilianza kunikata, nilighafirika na kuamua kukata simu kisha nikaanza kumwaga machozi  nikiwa pale kwa mwenye kibanda cha simu.

Alinishangaa sana Yule kaka ambaye alikuwa anatoa huduma ya simu, akaniuliza nini ambacho kilikuwa kimenisibu, sikuweza kumwambia  kisha nirudi tu kijijini, siku zilipita bila Maiko kunijulia hali, nishangaa sana hata mama yangu nahisi naye alishituka kuwa pengine kutakuwa na kitu, alimua kuniuliza, vipi tena mwenziyo mbona simuoni au hujamwambia kuwa una ujauzito.
Mama aliniuliza, nikamdanganya kuwa siku ile niliyoenda center kumpigia simu hakuwa anapatikana hivyo nitaenda siku nyingine.

Siku mbili zilipopita mama alijichangachanga pesa kidogo aliyoipata kutokana na kufanya vibarua vya kuvuna karanga kwenye mashamba ya watu wengine na kunipa ili nitumie njiani kama nauli.
 Nilifika hadi eneo la kibanda kile na kuomba muda wa kuongea  nikapewa, nilimpigia Maiko alipokea kwa kana kwamba alikuwa ana hasira na mimi au hakutaka kupokea simu yangu.

 “Unasemaje. Mbona wewe msumbufu sana,”alisema Maiko.
Nikabaki nashangaa leo hii mimi nimekuwa msumbufu kwa Maiko, inakuaje, nikawa nahisi sijielewei elewi vile. Nilimwabia Maiko samahani sana kama kuna jambo nitakuwa nimekukosea, ila nafahamu sijakosa chochote.
“Haya sema haraka bhana mimi nina kazi nyingi za kufanya,’ alinijibu.

Maiko, mimi sijisikii vizuri kwa sasa, kabla hata sijamaliza alinidaikia jukwaju sasa mimi nifanyeje. Maiko nina mimba yako, tangu siku ile ya mwisho tulipokutana faragha sikuziona siku zangu.

“Sikiliza Kecho, naona unataka kunizoea si ndiyo, nani aliyekwambia anahitaji mtoto, kwa sasa mimi sijajipanga, cha kufanya huyo mtoto chukua kama zawadi yako,” kisha akakata simu huku akiachia bo nge la mfyonzo.

Niliumia sana sikuamini kama nimeingizwa kingi kirahisi hivyo na mbaya zaidi mimba juu,  nilijiuliza ni kwa namna gani nitamwambia mama yangu na anielewe, maskini mama alijitolewa kunipatia nauli ili nikaonane na mtu ambaye aliamini ni muungwana, babamkwe wake lakini kumbe ni mtu katili.
Niliamua kurudi nyumbani huku nikiwa nalia njia nzima, niliona kama nimejiabisha sana pale kijijini na kuwaabisha wazazi wangu. Mbaya zaidi kuna vijana ambao walikuwa wananitaka lakini niliwakataa kwa sababu tu ya Maiko.

Usikose kufuatilia nini kilifuatia baada ya msichana Kecho kufika nyumbani kwao.

Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U.
      edit