Hatimaye Wakristo na wasiyo Wakristo duniani kote leo wanasherehekea Sikukuu ya Krismas
(kuzaliwa kwa Yesu Kristo).
Wiki kadhaa ndugu zetu
waislamu walisherehekea pia Sikukuu ya Maulidi au kuzaliwa kwa Mtume Muhammad
(S.A.W), walimaliza salama na Mungu awaongoze Wakristo nao wamalize salama
sherehe hiyo.
Msimu wa sikukuu huwa kuna
mambo mengi sana ambayo hutokea katika jamii yetu, kuna watu wanageuza sherehe
hizi kuwa za kulewa, kuzini, kugombana, kufumania, kuchinjana, kutukana na
mambo mengine mengi yenye uovu ndani yake.
Kama huu miongoni wa watu
hao achana na mambo haya, jipange kwa ajili ya mwaka mpya wa 2017. Jiulize
umelumbana mara ngapi na mpenzi wako au mumeo, umepigana na walevi au wahudumu
wa baa mara ngapi, jitathimini umetukana na majirani zako mara ngapi?
Jiulize, umekoswakoswa
kuuwawa kwa tuhuma za wizi mara ngapi? Umedundwa na kusutwa kazini na mtaani
mara ngapi? Umefumaniwa na mpenzi, mchumba, mkeo au mumeo mara ngapi na kwa
nini?
Kama ni mtu ambaye
unapenda maendeleo ya familia au mpenzi wako basi ukishapata majibu ya maswali
hayo anza kujifanyia tathimini ili kupunguza au kuachana kabisa na tabia za
kishenzi shenzi ulizonazo, ili ujipange kwa ajili ya mwaka 2017 ili uwe wa
mafanikio kwako.
Jiulize ni kwa kiasi gani
umerudi nyuma kwa sababu ya mambo yasiyokuwa na maana kwako, mara ngapi familia
yako imelala njaa kwa sababu tu ya uzembe wako wewe mzazi, iwe wa kike au wa
kiume.
Yawezekana umefeli sana
katika mitihani yako, maisha au biashara zako, pengine umefeli na sana katika
mahusiano yako, kila mwanaume au mwanamke unayempata hamfiki naye mbali aidha
kwa sababu yako au yake.
Bado haupaswi kujilaumu,
kiukubwa ni kujifunza, kukubali ukweli kuwa umeachwa au umeachika kisha anza
maisha mapya, jipange namna ya kuweza kutoboa.
Aijalishi kama mchana au
usiku wa leo hauna uhakika wa kula , jiamini unaweza kubadili maisha yako
kutoka hapo ulipo hadi kufikia huwa mtu mashuhuri, maarufu au staa.
Kama ni mfanyabiashara jiulize
ni kwa nini umeshindwa kupiga hatua, nawe msanii basi jipange kwa ajili ya
kujitangaza kitaifa na kimataifa,(M&U tutakusaidia kukupa ushauri na
chaneli zingine)kama ni mkulima hakikisha unalima kilimo chenye tija, kama ni
mwandishi basi hakikisha unaandika makala zenye kuwajenga Watanzania
wanaokusoma, kama ni mwalimu hakikisha unatimiza wajibu wako vizuri ili mwisho
wa siku upate kula matunda.
Mwaka 2017 ni mwaka wa
mabadiliko kwako, rekebisha mapito yako mabaya uliyoyapitia, usijilaumu kwa
kile kilichotokea katika maisha yako. Usijione kama umechemka au umekosea sana,
hapana ulikuwa mafunzoni, sasa umeiva anza kufanya yaliyo mema.
Ebu jaribu kutafakari ni
kwa nini watoto wako tu wamekuwa wakirudishwa nyumbani kwa sababu ya wewe
kukosa ada wakati watoto wa jirani yako wanaenda shuleni kama kawaida. Siajabu
hata mshahara na cheo unamzidi huyo jirani.
Funguka ndugu yangu, mwaka
2016 fanya kama ulikuwa wa mwaka wa mwisho kwa wewe kufanya mambo yakipuuzi,
fanya kama ulikuwa kwenye mapito na sasa umegundua zuri na baya.
Piga goti chini na mlilie
Mungu akufanye kuwa mtu mpya kwa mwaka ujao, akuepushe na migogoro ya kila siku
kwenye ndoa au penzi lako akuepushe na mabalaa ambayo umekuwa ukikuitana nayo
kazini na kwenye biashara zako.
Mwambie ALLAH umechoka kuitwa
mgumba wakati kwenye vitabu vitakatifu aliweze kumpa ujauzito mama mzee ambaye
alionekana ni tasa. Mwambie Yehova umechoka kusumbuliwa na magonjwa sugu wakati
yeye ni mti wa uzima.
Mwaka 2017 jitahidi
kujirekebisha na kukaa karibu na MUUMBA WAKO. Kwa naishi hapa.
Uongozi wa M&U
FOUNDATION unapenda kukutakiwa Krismasi na Mwaka Mpya mwema.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. iunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745.
Unaweza
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea
ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U