Saturday, December 17, 2016

Published 12/17/2016 11:00:00 PM by

USHAURI WAKO: MKE WANGU KANITELEKEZA NA WATOTO!





Mara nyingi imezoeleka kuwa mwanaume ndiyo huwa anakimbia au kutelekeza familia yaani mke na watoto, lakini kwangu mimi mke wangu ndiyo kanitelekezea mimi na watoto wake mwenyewe aliowazaa.
Mimi ni baba wa watoto wawili, nilimuoa mke wangu kwa ndoa kabisa na hadi sasa tulikuwa na zaidi ya miaka 8 kwenye ndoa.

Maisha yetu yalikuwa ni mazuri tu, ila baada ya uchumi wangu kuanza kuyumba, nikamuona kama ameanza kubadilika, nilijitahidi sana kumsihi na kumshirikisha katika mihangaiko yangu ilimradi tu asikate tamaa. Kwani kuna kipindi hata mlo wa siku.
Nilihisi kuwa kumshirikisha kutamfanya asipoteza matumaini na mimi au maisha yetu kama ya awali, kumbe nilikuwa najidanganya,  niliamka na kwenda kazini kama kawaida lakini niliporudi sikumkiuta, nilivyochunguza mule ndani mwetu niligundua kuwa kabeba baadhi ya nguo zake.

Nimeumia sana, inamaana mke wangu hataki shida, aamini kama kuna shida, je, huko alikokimbilia uchumi hauwezi kuyumba kama wa kwangu. Nimebaki njia panda niko na wanangu, naombeni maoni yenu tafadhali.

Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na :M&U
      edit