Nilipoishia wiki ……
"Kama kweli Maiko unanipenda basi
njoo nyumbani japo ujitambulishe ishu ya mahari siyo tatizo, unaweza kuongea na
familia yangu watatuelewa." Binti alimwambia Mpenzi wake.
Maiko alikubali na kumwabia binti kuwa
atafikiria kuhusua suala hilo la kujitambulisha kwa wazazi wake.
Endela nami……
Siku kadhaa zilipita huku tukiendela
kuwasiliana, Maiko akionesha ukaribu ambao nilizidi kumuamini, na mwisho wa
siku alikutana familia yangu akiwemo mama mzazi na baba yangu wa kufikia.
Walimkubaliana na kumpa utaratibu mzima,
alikubali na kuahidi kutekeleza kila kitu ikiwemo kutoa mahari.
Nilimwamini Maiko kama mwanaume wangu wa pekee
katika maisha yangu ambaye amejitolea kunipenda kwa dhati na ndiyo maana
ameenda hadi nyumbani kwetu kuzungumza na wazazi wangu, nilifurahi sana,
nilizidi kumpenda mno Maiko.
Sikuona sababu za kumbania kumpa tunda la
roho ingawa sikutaka kumuonesha kuwa niko tayari amege tunda langu, ila moyoni
nilimwamini na nilikuwa tayari kumpa utamu wangu, muda wowote na sehemu yoyote.
Hatimaye Maiko akapeleka kishika uchumba,
nikahisi sasa nimeishakuwa mke wa mtu, nikamkabidhi moyo wangu kijana Maiko.
Nakumbuka ilikuwa ni Jumamosi moja hivi
akaniomba tukutane Jijini Dar, nikakubali, nikawaga wazazi wangu kuwa naenda
kwa mwenzangu wakakubali.
Je, nini kilifuatia huko Jijini Dar
alikoenda kukutana na mpenzi wake, Maiko? Usikose sehemu inayofuatia ya mkasa
huu kila Jumapili na Alhamisi saa 9 Alasiri.
Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI,
MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa