Monday, December 19, 2016

Published 12/19/2016 02:00:00 AM by

MKASA WA KWELI: NIMEAMUA KUJIUZA!-3



Nilipoishia wiki ……
Nilikutana na Maiko katika gesti moja iliyopo maeneo ya Mabibo jijini Dar, tukafanikiwa kuanza uhusiano wa kimapenzi rasmi, kama mtu na mchumba wake. 

Nilitembea na Maiko mara kadhaa, hatimaye nikaanza kuona mabadiliko katika mwili wangu kwanza sikuweza kupata hedhi, nikawa najiuliza nimekuaje, nilikua sijui namna ambavyo mimba inaingia na kusababisha hicho ambacho nilikiona kwangu.

Sikumwambia mama yangu mapema nilichofanya nilijaribu kuwadadi wanawake ambao wananizidi umri, wengine walinielewesha wengine walinishushua kuwa tayari nimenasa.

Niliendela na hali ile huku mwili nao ukianza kubadilika, mara muda mwingi nikawa nahisi uchovu tu, nikilala mara nageuka hivi mara vile ilimradi kero tu.
Mwisho wa siku ile hali ilinichosha na nikaamua kumwabia mama ukweli, kuwa mimi mwanaye yatari nimenasa, mama hakushangaa sana si unajua watu wa kijijini, basi aliniambia niwasiliane na mwenzangu kuhusu taarifa hizo njema.

Nilifurahi sana moyoni mwangu kwani niliona nitakuwa nimekamilika kuitwa mwanamke wa ukweli kwa kupata mtoto, na tena mchumba wangu Maiko atanipenda sana kwa sababu huwa nasikia baadhi ya wanawake ambao wanakuwa hawana uwezo wa ubeba ujauzito hunyanyasika sana kwa waume zao na hasa mawifi mtu.

Niliamua kutoka pale kijiji hadi eneo la center kwa ajili ya kumpigia simu Maiko kumfahamisha kile kilichotokea, nilipopiga kwa mara ya kwanza simu yake ikawa inaita tu, nikapiga tena na tena.

Nikiwa nimeishaanza kukata tamaa na kuhisi labda pengine mchumba wangu Maiko atakuwa kwenye matatizo, ghafla nikaona amepokea, ila nikastaajabu akiniuliza swali ambali sikulitegema kulisikia kutoka katika kinywa chaka hasa ukizingatia tulikuwa na muda mrefu hatujawasilia.

Je, unajua binti huyu aliulizwa nini na mchumba wake, usikose Siku ya Jumapili kuanzia saa 9 alasiri.

Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa


Na:M&U.
      edit