Utafiti wa
hivi karibuni umeonyesha kuwa wanawake wanaotoka mikoa ya kusini
wanazaa watoto wachache zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine. Aidha
utafiti huo umetaja kuwa wanawake wa Dar es salaam wanazaa wastani 3.8
mpaka 4.2 ikilinganishwa na mikoa mingine ya Kagera, Kigoma ambayo huzaa
wastani wa watoto 6.8.
AyoTV na millardayo.com imempata Dk. Heri Tungaraza
kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili kaeleza sababu zinazopelekea
wanawake wa DSM kuwa na watoto wachache ikilinganishwa na mikoa mingine.
‘imechangiwa
sana na namna familia zetu ambavyo zimejitahidi kufanya uzazi wa
mpango, watu wameamua kupunguza idadi ya watoto kimakusudi kutokana na
sababu za uelewa na kutaka kubadilisha staili za maisha’-Tungaraza
Source: Milardayo.com
Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA
MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge
na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea
ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza
Hapa