Friday, February 24, 2017

Published 2/24/2017 12:00:00 PM by

ALINITONGOZA NIKIWA DARASA LA PILI, AKAOA, LEO ANATAKA KUNIOA!

Nilikuwaga na boyfriend wangu ambaye alianza kunitongoza tukiwa darasa la pili ila mimi nilimkatalia, nilipofika kidato nikamkubalia tukawa wapenzi.

Aliendelea na shule lakini alipofika kidato cha pili akaniambia muda si mrefu ataacha shule na kweli, aliacha.

Baadaye alikamatwa akiwa na binti mwingine, wazazi wa yule kijana wakaenda kutoa mahari kwao na binti, wakaoana.


Nilikutana naye boi wangu akaniambia kuwa alioa mwanamke ambaye si chaguo lake, kwa sababu alilazimishwa ila mimi ndiye chaguo lake hasa.
Aliishi na yule mwanamke kwa miaka mitatu wakapata mtoto mmoja, sijui nini kilitokea kati yao yule mwanamke akatoroka kwa jamaa.

 Sasa yule mwanaume amenifuata na kuniambia kuwa mimi ndiye mke wake anayenipenda na anataka kunioa, niko njia panda. Naomba ushauri wako?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U


      edit