NILIPOISHIA…
Haya ndiyo maisha ya wanawake wengi
duniani, wapo ambao wanapana nafasi ya kuyasimulia kama mimi lakini wengine
hawapati kwa sababtu hawajui wapi kwa kuanzia, hawafahamu nani ni sauti yao.
ENDELEA…
Nilitafakari sana juu ya misukosuko
ninayoipitia kwenye maisha yangu, nilimuona Maiko ni kama chanzo cha matatizo
yangu yote, nilimuona Minza kama mnyama mkali asiye na huruma, ni mwanadamu
ambaye anatabia za kinafiki kwa sababu alishindwa kuniambia kama amenichoka na
matokeo yake ameniazishia visa vya hapa na pale, kiasi cha kuniandalia watu wa
kunibaka.
Nilijiuliza itakuaje kama Minza akija
kubaini kuwa lengo lake la mimi kubakwa na wahuni halijatimia si ataanza
mipango mingine kimyakimya ya kunitoa uhai wangu.
Kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa
kiza, kwani nilicheka, nilikula na kulala naye kumbe akilini mwake ana jambo
mbaya.
Baada ya siku kadhaa Minza akajifanye
amerudi kutokana safari, na mimi sikumwambia wala sikuonesha dalili zozote
kuhusu kunusurika kubakwa na wahuni aliowaandaa.
Lakini moyoni mwangu nilikuwa namuogopa
sana kusema kweli, na nilijifunza kumbe mtu anaweza kukuchekea usoni kumbe
moyoni mwake ni adui wako namba moja.
Niliendea na maisha ya kwa Minza kibishi
nikiwa sina namna zaidi ya kuvumilia ingawa aliongeza chuki zaidi zidi yangu.
Sijui kama aligundua kuwa lengo lake
halikutekelezwa au lah, baadaye nilipata mwanaume mmoja ambabaye alikuwa ni
dereva basi tukaanzisha mahusiano yale.
Nilimsimulia mambo mengi sana kuhusu
mapito na matatizo yangu, na yeye
alionekana kuguswa sana na kuahidi kunisaidia.
Je, dereva ambaye amempata Kecho ataweza
kumsaidia matatizo yake ikiwemo na mtoto wake kunyooshwa mguu?
Usikose
kesho muda kama huu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U