Nina
kila sababu ya kumshukutu Mungu kwa wema wake, kwa kunipa na kukupa nafasi wewe
msomaji wangu kujumuiika name katika kuelimishana juu ya maisha na mahusiano.
Mada
ya leo inazungumzia kwa wale ambao waliamini au wanaamini kuwa ndoa ni jambo la
kawaida ni kama kwenda kununua nguo kwenye Soko la Kariakoo na kuvaa
lakini fasheni yake ikipita basi unalitupa kule au unaligawa.
Ndugu
yangu, ndoa siyo ya hivyo, ndoa ni mkataba wa maisha, mkataba wa kudumua na
kuvumiliana kwenye shida na raha.
Uzuri
wa mapenzi bana ukishaingia umeingia, haijalishi uliingia kwa mtindo upi, kitu
kikishakukolea hata ufanyaje?
Siku
ya leo napenda kuwashauri sana wale ambao wako nje ya ndoa kuwa ndoa siyo nguo
useme unaweza kuinunua ukaivaa na baadaye ukaiacha au kuijaribisha, ndoa ni
kiapo, tena kiapo cha kifo hasa, kwani mnashauriwa ili kuacha basi ni hadi pale
Mola anakapomtwaa mmoja wapo. Ingawa inawezekana kiapo hicho ni tofauti kwa
imani zingine lakini sehemu kubwa ndoa ni muunganiko wa jinsia mbili tofauti
ambazo zinaungana na kuwa mwili mmoja.
Jambo lako ndiyo la mkeo, la mumeo ndiyo lako,
hiyo ndiyo maana ya ndoa, kisha yanafuatia mambo mengine kama kusaidiana, mambo ya kawaida na hata yale ya kimapenzi.
Wasaa
wangu kwako ambaye bado hujafanikiwa kuoa ni kuwa makini sana na uchaguzi wako,
ni kuwa makini sana na mtu ambaye unataka kuingia naye kwenye kiapo cha maisha
yako.
Usikurupuke
kwa sababu jamaa anaonekana ni HB, achana na urembo wake, weka pembeni hako
kagari kake alikoguja nako nyumbani kwenu, kwanza yawezekana kakaazima, ka dada
yake au shemeji yake au kakodi ilimradi akutie roho juju tu mtoto wa watu.
Achana
na kazi au elimu nzuri aliyonayo, mwanaume au mwanamke wa ndoa hachaguliwi kwa
mtindo huo, hachaguliwa kwa kuangalia vigezo hivyo bali ni lazima uijikridhishe
je, ana vile vitu unavyovihitaji katika maisha yako.
Kama hana basi huyo
hakufai maana itafika sehemu unamuacha au utamtafutia sababu za hapa na pale
ili muachane, kwa mfano unapenda mwanamke au mwanamu ambaye ni mpole, basi
tafuta mwanaume mwenye hulka na tabia hizo ili uishi katika ndoa ambayo
unaipenda. Lakini ukiolewa ilimradi umeolewa nakwambia itakukosti baadaye.
Vijana
wengi wa sasa wanachagua watu wa kuishi nao kama wanandoa kwa sababu ya kitu
Fulani na ndiyo maana baada ya muda
Fulani unasikia ndoa ile ambayo ilivunja rekodi kijijini imevunjia, ukichunguza
kwa ndani imevunjika kwa sababu kile kilichowaunganisha kimeisha au kimepotea.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U