Monday, February 6, 2017

Published 2/06/2017 12:00:00 PM by

KWA TABIA ZA MUME WANGU, NAHOFIA KUMBEMENDA MWANANGU



Naitwa Jesca ni mama wa kitoto kichanga cha miezi 6, mwanaume ambaye naishi naye alinitorosha tu , kwani ndugu zake na wangu hawafahamu rasmi  mahusiano yetu, ila kuna mtu mmoja kwao huwa nawasiliana naye anayedai ni shangazi yake.
 
Tunaishi mkoa mwingine na mkoa wetu, ila mwanaume wangu hutumia vilevi mbalimbali ikiwemo pombe, sigara na hata wakati mwingine huwa nasikia harufu ya bangi kutoka kinywani mwake. 

Kinachonishangaza akilewa anataka kuniingilia faragha bila maandalizi yoyote jambo linalopelekea kuumia sehemu za siri na kutokuhisi kabisa raha ya tendo hilo.

Mbali na kuniingilia kwa nguvu nimemwambia kuwa mtoto wangu bado mdogo tunaweza kumbemenda hanielewi, najuta kuishi na mwanaume huyu.
 
Kwani kwa tabia yake ya ulevi na kutaka ngono sijui huko anakuwa huwa anatembea na nani, wasiwasi wangu ni kwa mtoto wangu.

Nimejaribu kumshauri sana kuhusua suala hilo lakini hanielewei, imefika sehemu mapenzi kwangu ni kama mateso. Naombeni ushauri wenu wadau wa M&U.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U


      edit