ULIPOISHIA…
Umati
ule wa watu nikaanza kuuoa kama vile unapepesuka, mara taswira za watu wale
waliokuwepo eneo la tukio zikaanza kupotea katika fikra zangu kiasi cha
kushindwa kumtabua nani ni nani?
ENDELEA…
Kecho baada ya kuanza kutokewa na hali ile
ya kushindwa hata kuwatambua watu waliokuwepo kwenye tukio la ajali. Mara
alianza kupepesuka na mwili nguvu kumuisha kisha mwili mzima ukalegea na
kujiachia kwa kudodoka, bahati nzuri kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa
amegeuka kumuangalia wakati anapiga kelele za kilio.
Kabla hata ajafika chini akawa amedakwa na
watu watatu na kuwekwa pembeni, wakina mama wawili akiwemo jirani yake wakavua
kanga zao na kuanza kumfunika ili asimwage radhi pamoja na kumpepewa kwa ajili
ya kumsaidia kupata hewa safi zaidi.
Maskini Kecho alikuwa amepoteza fahamu
kutokana yeye kushuhudia mwili wa Jakobo ukiwa umekanywaga na gari. Alilia sana
inavyoonekana alimua zaidi ndani kwa ndani kutokana na tukio hilo.
Baada ya kuona wamempepea lakini harudii
na fahamu, waliamua kutafuta gari na kumkimbiza haraka katika Hospitali ya Mkoa
wa Pwani ya Tumbi kwa ajili ya matibabu zaidi.
Walipomfikisha wauguzi walileta machela ya
kusukuma kwa ajili ya wagonjwa wasiojitambua kisha akawahisha haraka katika
chumba cha dharura na kuwekewa drip. Wauhuzi wa Hospitali ya Tumbi waliwahisha
machela hile kwa kufahamu kuwa yawezekana ni manusura wa ajali kwani hospitali
hiyo ni msaada mkubwa sana kwa majeruhi mbalimbali wa ajali zinazotokea katika
Barabara ya Morogoro.
Ilichukua kama saa kadhaa ndipo Kecho akarejewa na fahamu tena, kilichowashangaza
wauguzi na jamaa waliomleta ni kuamka na kuanza kuita jina la Jakobo,
aliwauliza ‘’Hapa niko wapi, nimefikaje, mwanangu na Jakobo wako wapi?
Muuguzi alimsogelea na kumbembeleza kwa
sauti ya ukarimu kuwa atulie kila kitu kiko sawa, mwanaye yuko kwa Minza ambaye
ni rafiki yake na Jakobo yuko salama. Waliamua kumdanganya kwa kuhofia
wakimwabia ukweli pengine angeweza kupoteza fahamu kwa mara nyingine tena.
Nini
kilifuatia? Mpenzi msomaji usikose kesho kuanzia saa 8 mchana kujua undani wa
mkasa huu wa kweli na wenye mafunzo ndani yake.
Kwa Ushauri Wa
Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na
Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745
au 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U