NILIPOISHIA….
Mamaa yangu weeeeeeh! Sikuamini macho
yangu kwa kile nilichokiona, sikuweza kuvumilia zaidi ya kulipukwa na kilio kwa
sauti kubwa na ya juu sana. Sauti ambayo kila mtu aliyekuwepo eneo la tukio
ilimradhimu kutaharuki na kugeuka, kunitazama “Mama yanguuuu jamani Jakobo,
Jakobo weeeeeeh!”
Kwa kilio kile, Kila mtu alibaki
akinishangaa mimi, wengi walitaka kujua nini kinachoniliza, je, nina undugu
wowote na marehemu?
ENDELEA NAMI…
Watu waliendelea kujiuliza yule mtu
aliyegongwa na kufariki dunia alikuwa ni nani kwangu, kama ni nina mahusiano
naye ni ya aina ipi? Kwa maana nilionekana kuguswa sana na tukio lile. Wengi
walikuwa wakiniona nikienda kushuhudia na kuwasaidia wamjeruhi na wengine
waliokuwa wakipatwa na ajali eneo lile lakini sikuwa nalia kama ambavyo nililia
siku hiyo.
Najua maswali mengi sana yaliusumbua umati
ule mkubwa kutokana na namna nilivyolia, tena kilio chenyewe kilikuwa ni cha
sauti kuu, sauti iliyojaa uchungu ndani yake, uchungu uliojaa malalamiko,
malalamiko yaliyoonesha kukata tamaa ya maisha kwa sababu tu nuru ambayo
nilikuwa nimeanza kuipata katika giza nene (maisha yangu), nililokuwa nalo,
nayo imetoweka ghafla, bila kufikia ndoto zangu au zile ambazo zilikuwa
zinatakiwa kutekelezwa.
Nililia kwa uchungu mkubwa sana, na hakika
kabisa katika maisha yangu sijawahi kulia kama siku hiyo niliposhuhudia yule
mtu akiwa amekanyagwa na gari na kusambaratishwa mwili wake, damu, ubongo ukiwa
umetapakaa huku na kule karibu eneo lote la barabara, niliumia sana, nilisikitika
sana, nilivunjika moyo na kunyongonyea haswa, kwanza sijawahi kuona ajali mbaya
kama ile pamoja na nakushuhudia ajali nyingi katika eneo lile.
Nilianza kuhisi mwili wangu wote ukiishiwa
nguvu, sauti ya kilio changu ikaanza kupungua kutoka sauti ya juu niliyokuwa ninalia, ikawa inapungua
kadri muda ulivyoenda, macho nayo
nikaanza kuhisi yakipoteza mwagaza wa jua kali lililokuwepo eneo la tukio.
Ghafla sauti yangu ikakata kabisa kusikika
ila kwa akili niliyobakiwa nayo, kwa mbali nilihisi midomo yangu ilikuwa bado
inaweza kufunguka kwa kulia lakini sauti haikuweza kutoka kama awali.
Umati ule wa watu nikaanza kuuoa kama vile
unapepesuka, mara taswira za watu wale waliokuwepo eneo la tukio zikaanza
kupotea katika fikra zangu kiasi cha kushindwa kumtabua nani ni nani?
Mpenzi msomaji nini kilifuatia kwa Kecho
baada ya kuanza kutokewa na hali ile ya kushindwa hata kuwatambua watu
waliokuwepo kwenye tukio la ajali.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U