NILIPOISHIA…
Kutokana na wiki nzima kukaa bila kunyonya
kutokana na mimi kuzimia basi mama alinishauri nimuachie moja kwa moja.
Nilifanya hivyo. Nilirudi geto kwetu kwa Minza na kuendelea na maisha kama
kawaida
ENDELEA
NAMI…
Habari zilikuwa zilishatapakaa pale
kijijini kuwa yule mtu aliyegongwa
alikuwa ni mpenzi wangu, hivyo kila siku nilikuwa ni mtu wa kupokea salamau za
pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa pale Kwa Mafipa. Kiukweli nilitamani hata
wasije kwani wengine nilikuwa kama naona wananiongezea tu machungu kutokana na
maneno yao ya pole.
Maisha yalianza kuwa magumu kwa mara
ngingine, nilianza kuhisi pengine nina mikosi na maisha haya, yawezekana
kuzaliwa katika familia ya kimaski ni ndiyo tatizo kwangu. Nililia sana kila
nilipomfikiria Jakobo kwani kwangu alikuwa ni msaada mkubwa sana.
Kipindi cha kulala njaa au kushindia mlo
mmoja kikawadia kwa mara nyingine, ugumu wa maisha ukaendelea kama kawaida
kwani pesa niliyokuwa nayo kama akiba, Minza aliitumia kunitibishia pamoja na kulipia
kodi ya nyumba kutokana na mkataba wa awali kuisha.
Miezi miwili ilipita bila kuchangia
mchango wowote wa chakula pale geto jambo lililomuudhi sana Minza na kuanza
kuniona mimi kama mzigo kwake, sina msaada wa aina yoyote kwani ananilisha,
ananilipia kodi.
Visa vilianza vya kila aina, sijui
alipatwa na nini Minza aligeuka sana , nikawa nikimuuliza kitu ananijibu kwa
jazba, mara anaanza tu kunifokea kama mtoto mdogo. Kuna siku nilichukia sana na
mimi hasira zikanishika.
Usikose
kujua nini kilifuatia baada ya Kecho kushindwa kuvumilia masimango ya rafiki
yake Minza.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U