Asante Mungu kwa Siku hii
ya Jumapili kwani nimeifika nikiwa salama na mwenye afya. Bila shaka hata nawe
mpenzi msomaji wa makala hii uu buheri wa afya. Pole sana kwa mtu ambaye
anasumbuliwa na matatizo ya aina yoyote ile. Pole sana uliyefiwa au kuuguza kwa
muda mrefu, usikate tamaa mgonjwa wako au wewe mwenyewe utapona ila mtegemee
Mungu kwa kila jambo.
Mada ya leo ni juu ya
kusudi la Mungu kwako wewe mwanadamu. Ndiyo maana kuna Maandiko Matakatifu yanasema
mwili wako ni hekalu takafitu.
KAMA ulikua hujui kama
binadamu wote ni sawa basi jitathimini upya, kusudi la Mungu kukuweka duniani
ni lipi? Na kama amekuweka bila kusudio kwa nini baadaye.
Umeshawahi kujiuliza kuwa yawezekana wewe
ndiye suluhisho la mgogoro wa madaraka unaoendelea nchini Gambia lakini
hujajifahamu na hutaki kujifahamu au kujigundua.
Siku zote Mungu huwa ana
makusudi na watoto wake, kwani ni kwani MUNGU pekee ambaye anauwezo wa
kumkweza mtu ambaye amekuwa
akidharauliwa kwenye familia, shuleni, kazini au kwenye jamii yake.
Lakini kwa maajabu ya
Mungu mtu huyo umkweza na kumpandisha na watu kuanza kujiuliza na kuanza
kumsemea mambo mengine mengi, ikiwemo ujambazi, ushirikina na kadhalika lakini
kumbe si kweli Mungu wake kamsimamia na kuamua kujidhihirisha kupitia yeye.
Jaribu kujichunguza upya
katika maisha yako, yawezekana Mungu ana mpango mzuri na wewe ila ameamua
kukupitisha kwenye shida, changamoto ili ujue shinda na matatizo ya wengine ili
siku akikupandisha basi uwasaidie watu wake kwa sababu unafahamu hali zao.
Yawezekana wewe ndiye tiba
halisi ya ugonjwa hatari wa zika, malaria, pepopunda, Ukimwi na mengineyo.
Yawezekana wewe ndiye suluhisho la ajali nchini au duniani, yawezekana wewe ni
chanzo cha upatikanaji wa nishati ya umeme yakudumu. Inaweza kuwa wewe ndiye
msuluhishi mkubwa wa nchi zinazopigana vita kila kukicha.
Jiangalie labda pengine
wewe ndiye tabibu wa wanawake wanapatwa na kifafa wakati wa kujifungua,
yawezekana wewe ni suluhisho la kilimo cha kusubiri mvua, yawezekana wewe ni
mmoja ya watu ambaye unaweza ukatengeneza ajira nyingi duniani.
Yawezekana wewe ndiye
suluhisho la elimu ya Kitanzania kuitoa hapo ilipokuipeleke levo zingine, labda
wewe ndiye mgunduzi wa mitambo f’lani ambayo inaweza kuisaidia jamii kujikinga
na ajali, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, vikongwe wanaouwawa kwa
kukatwa na mapanga.
Hivyo huna haja ya kukataa
tamaa kwenye biashara yako, kwenye uhusiano wako, kwenye uchumba wako, kwenye
ndoa yako na hata kwenye huo ugonjwa ambao unakusumbua kwa muda mrefu.
Mungu anajaribu
kukupitisha kwenye mapito ambayo yatakufanya ujue nani ni mtu mwenye msaada
kwako, nani anaupendo na wewe katika maisha yako, mpenzi wako yuko wakati wewe
ukiiumwa, au ukiwa na tatizo, je, anakupenda zaidi au anakuwa kama kakupotezea.
Amka sasa na ujipange
upya, Mungu hajakuleta duniani kwa ajili
ya kutesekana kusubiri kifo chako chenye mateso labda ya duniani na ahera.
Ni lazima anakusudi la
kipekee sana katika maisha ya kila mmoja wetu kama utajichunguza kwa makini
zaidi.
Achana na kuendelea kujiona
kwa duniani umekuja kimakosa au umeumbwa kuteseka, huteseki ila unapitia
majaribu ambayo yanakukomaza, majaribu ambayo ukiyashinda unakuwa mshindi siku
zote.
Kwa mtu yeyote mwenye
swali la kuhusu mapenzi au mada hii ya ujasiriamali basi anaweza kunitumia
inbox na atajibiwa.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U.