Monday, February 13, 2017

Published 2/13/2017 12:00:00 PM by

KISA PICHA YA UTUPU, KANICHUNIA.



Mimi ni mwanamke wa miaka 29, niliolewa kwa miaka kadhaa ila ndoa yangu ilivunjika mwaka 2015 baada ya kubaini kuwa mume wangu kazaa na msichana wa kazi. 
 
Mwaka jana nikakutana kijana ambaye nina mzidi umri kwa miaka 5, wote sisi ni walimu , tunafundisha shule moja mkoani Songwe.
Kijana huyo alinipenda na kuniahidi kunioa ila kabla ya yote alinipeleleza kwa kila kitu, anajua 

Kila kitu kuhusu maisha yangu, anajua akaunti
Yangu ina shilingi ngapi, nalipwa mshahara kiasi gani,  nadaiwa na nani na bei gani? Kwa kifupi alinipeleleza sana na mimi kwa sababu ya nguvu ya penzi nikaweka wazi kila kitu kwake.


Mwaka jana alipata nafasi ya kwenda kusoma mkoa mwingine akiwa kule aliniomba nimtumie picha ikiwa inaonesha mapaja yangu, sikumtumia basi ugomvi ukaanzia hapo.

Nikimipigia simu hapokei wala sms zangu hajibu, ila mimi bado nampenda. Swali langu je, huyu anafaa kuwa mume wangu au ni mzushi?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U


      edit