Tuesday, February 7, 2017

Published 2/07/2017 12:00:00 PM by

NILITOROSHWA NA MWANAUME, SASA NAYAONA MATESO!






Mimi ni binti, mwenyeji wa Mkoa wa Kigoma nilikuwa naishi na ndugu zangu baada ya wazazi wangu kufariki dunia, nilipata bwana ambaye tukawa naye kwenye mahusiano ila kumbe hakuwa mkazi wa Kigoma.
Nilijikuta nikikolea kwake na nikawa mtu ambaye sisikii ushauri wa mtu, sijui kama ni ujinga wa mapenzi au kuna vitu nilifanyiwa.

Baada ya kumaliza shughuli zake, yule kaka alinishawishi tuondoke wote kuelekea jijini Dar, nilikubali kwa sababu nilimpenda lakini nilikuwa na hamu ya kufika Dar.

Maisha ya Dar ni mabaya sana, kila siku aishi kunipiga na kunisimanga, kuwa sina msimamo kuambiwa tutoroke, name nikakubali.
Naumia sana, naona aibu hata kuwaambia ndugu zangu kwani walinishauri sana ila sikusikia. Ninyi wadau wa M&U ndiyo msaada wangu, naombeni ushauri wenu.
 
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit