Tuesday, February 7, 2017

Published 2/07/2017 02:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-32



NILIPOISHIA…

Baada ya mwili wa Jakobo kuhifadhiwa walitafutwa ndugu zake na kukabidhiwa mwili wa ndugu yao, hawakuwa wanafahamu kama kuna mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano na ndugu yako.



SONGA NAMI…

Hawakufahamu kama nilikuwa nimepoteza kumbukumbu kwa sababu ya mshituko wa kumuona Jakobo akiwa amefariki wa ajali mbaya.

Ndugu wa Jakobo walikaa vikao vya dharura palepale maeneo ya mochwari wakishauriana na kupanga mikakati ya namna ya kumzika mpenzi wangu. Baada ya kujadiliana kwa muda haimaye walikubaliana kuwa mwili wa Jakobo mpenzi wangu ulipaswa kusafirishwa hadi kijiji kwao Mwamgongo mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

Hatimaye mwili wa kipenziu changu ulisafirishwa kwa ajili ya safari, ndugu na marafiki walikuwa karibu walipata nafasi ya kuuga mwili wa Jakobo pale Tumbi lakini mimi sikuwa na nafasi hiyo, kwa sababu bado nilikuwa sijarudiwa na fahamu na hata kama ningekuwa nimerejewa fahamu zangu isingekuwa rahisi kwa wauguzi kuniruhusu kuuona mwili wake Jakobo labda kama wangeniruhusu kwa kuwa na machela palepale,  kwani nisingejiweza kwa lolote kuvumilia.

Mpenzi msomaji, pamoja na mapenzi na upendo wote ule wa Jakobo lakini sikuweza kumzika mpenzi wangu. Sikuweza kumuaga mwanaume ambaye alinipenda kwa dhati nami nikampenda kwelikweli.

Huo ndiyo ukawa mwisho wangu na Jakobo, akilini mwangu nikakumbuka ule msemo wa’ngombe wa maskini hazai,  kama akizaa dume ambalo nalo haliwezi kudumu.
 
Baada ya wiki moja kupita hatimaye nilirudiwa na fahamu zangu kama kawaida, niliruhusiwa kurudi nyumbani, alikuja mama, majirani  na rafiki yangu Minza akiwa na mwanangu Gift. Nilikuwa nimemkumbuka sana mwanangu.

Kutokana na wiki nzima kukaa bila kunyonya kutokana na mimi kuzimia basi mama alinishauri nimuachie moja kwa moja. Nilifanya hivyo. Nilirudi geto kwetu kwa Minza na kuendelea na maisha kama kawaida.

Nini kilifuatia baada ya Kecho kuruhusiwa kutoka hospitalini?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit