Imekuwa ni
kasumba kwa wapenzi wanaogombana au kulumbana kwa muda mrefu kwasababu
mbalimbali zikiwemo za uhusiano wenyewe, ugomvi wa ndugu wa upande mmoja,
kipato duni na mengineyo.
Mada yangu inazungumzia makosa yote kwa ujumla ambayo
inawezekana mwenza wako kayafanya, haijalishi amekuwa akifanya mara kwa mara au
lah! Nachozungumzia ni kosa ambalo linaweza kumkwanza yeyote aliyeko kwenye
uhusiano wa kimapenzi.
Angalizo:
Tabia hiyo siyo yakufanya hata katika maisha ya kawaida, haipendezi.
Kama mtu kakukosea, ukamwambia na mwisho wa siku
amekubali kosa na kutubu mbele yako, tena akiwa kapiga magoti huku akimwaga
machozi, kwa upendo na kuguswa na huruma yake dhidi ya kosa au kitendo
alichofanya ukaamua kumsamehe, kwa kumshika mkono na kumnyanyua sakafuni
alipopiga magoti, kisha kumkumbatia kwa ishara ya kumsamehe na bado unamwitaji
na kumpenda.
Napata wakati
mgumu sana naposikia au kuona umemsamehe mwenzi wako lakini kila akikukosea
kidogo una msengenya kwa kumkumbushia kosa au makosa aliyowahi kukukosea,
sidhani kama inapendeza sana, kama ulimsamehe kuna sababu gani? ya kumkumbushia
alichokukosea kama sio kumnyong’onyesha mwenzio na kujiona mkosaji siku zote.
Kwa tabia hiyo
ninaamini utakuwa unatumia nafasi hiyo kufanya maovu yako na kujikingia kwa
maovu ya mwezio, kwasababu tu kosa lake linafahamika.
Kama umeamua kumsamehe basi msamehe kweli toka moyoni,
na kama utamsamehe kwa maneno ni dhahili msamaha wako umejaa unafikri mkubwa
sana ndani yake.
Hivi ni maovu mangapi ya aibu na ajabu ambayo umekuwa
ukimfanyia mpenzi wako ila yeye hayajui!, umekuwa ukimsaliti na kumuabisha
mwenzio ila hajajua, sitaki kuamini kama wewe ni msafi sana kiasi kwamba huna
makosa, kujua kosa la mwenzio ndiyo imekuwa nongwa, kama umemchoka usitumie kuteleza kwake kama sababu ya wewe kumuacha,
kama unahisi huna mapenzi naye hakuna haja ya kuzunguruka na kumkumbusha mambo
ya miaka miwili iliyopita, wewe funguka bhana.
Ila kumbuka hata huko uwazako kwenda kuwa; Bucha ni
tofauti ila nyama ni ile ile, na kwa taarifa yako hata huko unakoenda
utaendelea na tabia yako kama kawaida na itakuwa ngumu sana kudumu na mpenzi
mmoja, kwasababu tu una roho iliyoinama wengine wanasema roho ya korosho au kwa
nini.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U