Ni kama simulizi lakini hii ndiyo hali halisi ya maisha yangu ya mapenzi.
Naitwa Ab ni mwanaume wa miaka 42 nilifanikiwa kumpata mwanamke wa miaka 37 mbaye nilimuoa kiaina kwa sababu hatujafunga ndoa. Nimeishi naye miaka 15 na tukabahatika kupata watoto watano.
Baadaye mke wangu alinitoroka akaenda kusikojulikana na hivi karibuni karudi akiwa na mimba ya mwanaume mwingine.
Ninaumia, ninateseka, sijui kipi nikifanye sahihi kwa tukio hili. Ndugu yangu unayebahatika kusoma ujumbe huu usipite bila kunipa ushauri wako kabla sijachukua maamuzi mabaya.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U