Friday, February 10, 2017

Published 2/10/2017 02:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-35


NILIPOISHIA…
Niliporudi nyumbani Minza hakuwa ananijali kwa lolote kwani aliendelea kuamini kuwa mimi ni mzigo kwake, basi akaamua kuniambia kuwa natakiwa nijiandae hivi karibuni mpenzi wake anakuja?

ENDELEA NAMI…

Nilijifikiria sana pa kwenda sikupaona nilichofanya ni kumwambia kuwa haina shida, nitajitahidi kutafuta kwa kujihifadhi wala asijali.
Siku ambayo Minza alisema kuwa bwana ake atakuwa amekuja, ikafika, lakini sikuona cha mwanaume wala dalili zozote kwa Minza kusema akijianda kumpokea. 

Vivyo hivyo kesho na hata kesho kutwa yake, naamini alishindwa kunitimua moja kwa moja ila alichokuwa anakifanya ni kunitafutia na kunifanyia visa ili niondoke mwenyewe.

Siku zikasonga tukiwa tunaisha kwa shida shida hivyo hivyo, nilijitahidi kumzoea kwa sababu sikuwa na namna ya kufanya ila ukweli niliumia sana kuna wakati nilikuwa najificha sehemu nalia weeeee, hadi nachoka kuisha narudi nyumbani nikiwa kiaina kidogo.

Baada ya siku mbili Minza aliniaga kuwa anakwenda kijijini kwao na atarudi baada ya siku tatu, nisiwe mnafiki nilipumua niliona kama hizo siku tatu ni heri zingejiongeza na kuwa mwaka ili angalau nipumzike na masimango ya Minza.
Pamoja na mimi kuwa nilisaidia pale kwa minza lakini nilikuwa nimeishachoka kutokana na tabia zake na laiti kama ningekuwa na pa kushika basi nisingeng’angania kuendelea kuishi naye, ila sikuwa na pa kwenda, nikaona niwe tu na kiburi cha kujilazimisha.

Ikiwa nimepita siku moja baada ya Minza kuondoka, nikiwa niko nyumbani na mwanangu nakoroga uji, mara nilishangaa vijana watatu wakawa wameniibukia tu vupu! Sikujua ni wapi ambapo walikuwa wametokea kwani sura zao kwangu zilikuwa ni ngeni kabisa.

Vijana hao ni kina nani na wanataka ni kwa Kecho na kwa nini waende usiku? Usikose kesho muda kama huu.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit