ULIPOISHIA…
Muuguzi alimsogelea na kumbembeleza kwa
sauti ya ukarimu kuwa atulie kila kitu kiko sawa, mwanaye yuko kwa Minza ambaye
ni rafiki yake na Jakobo yuko salama. Waliamua kumdanganya kwa kuhofia
wakimwabia ukweli pengine angeweza kupoteza fahamu kwa mara nyingine tena.
ENDELEA…
Ilikuwa ni majira ya saa 6 mchana muda wa
kutazama wagonjwa, alifika Minza akiwa amembeba Gift mgongoni huku analia,
alipofika kwa Kecho akazidisha kulia na kuanza kumwambia Kecho kuwa Jakobo
muuza mkaa maskini amefariki dunia, kisha akaanza kulia tena, jambo
lililorudisha kumbukumbu za Kecho kuhusu tukio lile na yeye kuanza kulia kama
awali, huku akitaja jina la Jakobo.
Nililia sana tena kwa kilio cha kwikwi
basi nililia kiasi cha kupoteza fahamu tena, niliambia baada ya kupoteza fahamu
Minza na wengine walimkimbilia daktari na kumweleza kilichotokea na kumuomba
msaada wa kuniangalia.
Daktari aliamuru watu wote watoke na
kuwaacha wafanya kazi yao, wakaniwekea tena drip nyingine, waliwaita kina Minza
na kuwakataza kuniambia habari za Jakobo na ikiwezekana basi wanidanganye hadi
pindi hali yangu itakapotengemaa.
Muda wa kuoa wagonjwa ulipoisha wakaondoka
na kurudi nyumba huku wakiniacha mimi nikiwa bado sijarudiwa na fahamu. Sikujua nini kiliendelea duniani. Kumbe
maskini mwili wa Jakobo ulichukuliwa na kuletwa katika chumba cha kutunzia
maiti cha pale pale Hospitali ya Tumbi.
Dunia katili sana, sikujua, nilikuwa sina
ufahamu wowote wa kutambua jambo lolote kwani ningejua ningeenda kumuaga mpenzi
wangu kwa mara ya mwisho, wema na upendo wake ambao alinionesha kwa siku chache
nilizofahamiana na naye hauwezi kujirudia kwa mwanaume yeyote yule katika uso
wa dunia hii.
Siku ya pili nikiwa sijarudiwa na fahamu,
ndugu yangu, mama na jamaa walikuja kunisalimia nikiwa sijitambui, mwanangu
Gift aliishi kwa maziwa na ng’ombe kwa sababu nisingeweza kumnyonyesha.
Baada ya mwili wa Jakobo kuhifadhiwa
walitafutwa ndugu zake na kukabidhiwa mwili wa ndugu yao, hawakuwa wanafahamu
kama kuna mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano na ndugu yako.
Je,
nini kilifuatilia, ndugu wa marehemu Jakobo waliweza kugundua kuwa Kecho ni
shemeji yao na kalazwa kwa sababu ya ndugu yao?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U