Naitwa M, niko Mbagala, jijini Dar nilikua na mchumba wangu
ambaye tulikuwa na malengo mengi tu ya kimaisha na katika mahusiano yetu ila
kwa sasa tumegombana kidogo.
Chanzo cha ugomvi wetu ni kutokana na tabia yake ya
ukorofi, bado hajanioa ila anagombana na ndugu na marafiki zangu. Imefika kiasi
nakosa amani na nina kuwa na maswali mengi sana kichwani mwangu kuhusu huyu
mwanaume. Je, ana mapenzi ya kweli? Na tukioana atawajali ndugu zangu kama sasa
hawajali?
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U