KWA mikono mikunjufu
kabisa napenda kukualika tena kwenye kujadili kuhusu mambo yanayokusibu kwenye
maisha ya uhusiano wa mapenzi na maisha ya kawaida.
Yawezekana umekata tamaa
na huoni mtu mwingine wa kumpa nafasi katika moyo wako kwa sababu tu
umeishaumizwa na kulizwa vyakutosha, umeishateseka sana kiasi ambacho umefika
sehemu huoni mwanaume au mwanamke mwingine ambaye unaweza kumpa moyo wako kwa
kuamini kuwa yawezekana na yeye ni wale wale webye kuumiza.
Ama kweli mapenzi fumbo la
ajabu sana katika mafumbo yote yaliyowahi kutokea duniani, fumbo ambalo
kulifumbua kwake ni ngumu. Na kama ni janga basi janga linalowaumiza vichwa
walio wengi ndani na nje ya uhusiano, wasomi na wasio wasomi, matajiri kwa
masikini, wenye akili na wasio na akili, wastaarabu na hata watukuti kwani wapo
wanaotamani kuingia penzini huku wengine wakipigana kufa na kupona kujinasua
katika penzi hilohilo lakini nadhiri ikiwasuta na kuwakatalia.
Najua unaona hakuna
mwingine wa kumpa moyo wako kwa sababu tu uliyempa awali alikuumiza, alikutesa,
alikuliza, alikusimanga, alikunyanyasa kisa kikiwa ni mapenzi, penzi lake
ambalo ulilithamini na kulipenda lakini bado mwisho wa siku kimekuumiza vya
kutosha.
Yawezekana wewe ni mmoja
wa wale ambao nawazungumzia kwenye makala haya ambao wameumizwa na hawana tena
hamu na mapenzi, hawako tayari kabisa kuwa na mpenzi kwa kuhofia hata huyo
atakayempata ni kama aliyewahi kumuumiza. Tapeli wa mapenzi kama yule ambaye
alimwamini lakini mwisho wa siku akamtapeli kwa kushindwa kujua thamani ya
pendo lake kwake.
Uliteseka juu yake,
ulimsaidia sana pale alipokwama, ulijitoa alipokuhitaji, ulimpenda na kumfariji
alipohitaji farijiko lako lakini leo hauko naye tena, aidha kwa kukuacha,
kumuacha au kuachana kwa sababu tu umechoshwa na vioja vyake.
Ulimpa furaha alipokuwa na
huzuni, ulisimama pembeni ya ubavu wake mliopoenda dukani kukununua bidhaa,
ulimshika kiunoni mwake mlipokuwa bichi lakini yote hayo ni kama simulizi
iliyowahi kutokea ilihali wewe ukitamani ingekuwa ni tamthilia inayoendelea.
Wewe ni mmoja wa wale
ambao wamekuwa wakijiuliza kila siku kuhusu kukosa mtu wa kumpa moyo wako, au
umewahi kusikia rafiki, ndugu au jamaa yako akilalamika au kusema maneno hayo basi
tuma maoni kuhusu mada hii.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U