NILIPOISHIA…
Kiukweli nilishangaa Mungu wa ajabu kwani
wao wenyewe wakaanza kubishana na kutofautiana kabisa, wengine wakaitaka
wanaibake, huku yule kaka mmoja akionekana kupingana nao na kunitete kwa nguvu
zote.
Ghafla yule mkaka aliyekuwa ananitetea
aliingiza mkono mfukoni kisha akatosa kitu, ambacho sikuwa ni nimekifahamu
kabla.
ENDELEA NAYO…
Maskini yule kaka alionekana kuguswa sana
na mamabo yangu niliyomuhadithia, akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa noti ya
shilingi 5000 kisha akanikabidhi na kuniambia kuwa wao walikuwa wametumwa na
Minza kwa ajili ya kuja kunibaka kwani nimekuwa nikitumia vitu vyake bure.
Minza amefanya kila figisufigisu ili
niondoke lakini nimekuwa siyo muelewa hivyo kaamua kutumia njia hiyo ya
kunitumia watu wanibake. Yule kaka akanisogelea kwa karibu zaidi na
kuninong’oneza na kuniambia, tafadhali usimwambie Minza kuhusu hili, kuwa
hujabakwa, wewe akija mdanganye tu kuwa umebakwa ili ajue tumefanya kazi
aliyotuagiza wala usioneshe kuwa tuliongea na wewe.
Wakati anasema hayo yule mbakaji mwema,
wenzake walikuwa wamesogea kando kidogo na walionekana wakimsengenya mwenzao
kwa kukwamisha dili lao, walihisi labda jamaa kanizimikia ndiyo maana kafanya
vile.
Yule kaka aliondoka na mwenzake, huku
akili yangu ikiwa haijielewielewi kwa kile kilichotokea sikumbuki hata kama
niliivisha chakula na kula au lah!. Sikuamini kama Minza anaweza kunifanyia
unyama mkubwa kama huo kisa kukaa kwake, hata kama amenichoka ni bora
angeniambia mapema nikaondoka. Nilijiuliza sana vipi kama wale vijana
wangenibaka halafu mmoja wapo awe ameathirika si tayari na mimi ningekuwa
kwenye hatari zaidi.
Haya ndiyo maisha ya wanawake wengi
duniani, wapo ambao wanapana nafasi ya kuyasimulia kama mimi lakini wengine
hawapati kwa sababtu hawajui wapi kwa kuanzia, hawafahamu nani ni sauti yao.
Mpenzi
msomaji nasimulia mkasa huu ili wewe kama mzazi au mhusika, uwe mwanaume au
mwanamke unapaswa na kuna jambo utajifunza kupitia mkasa wangu. Tukutane kesho
kufahamu nini kiliendelea baada ya pale.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U