Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya Eden Bliss, Nairobi ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Wapendanao.
Harusi ya Anne na Wilson Mutura ya awali iligharimu dola moja pekee ya Kimarekani lakini sherehe ya sasa inakadiriwa kwamba imegharimu takriban Sh3.5 milioni (Dola 35,000).Pesa hizo zimegharimiwa na makundi mbalimbali yanayohusika katika uandaaji wa sherehe, ambayo yaliungana kwa pamoja na kuchanga pesa kuandalia Anne na Wilson sherehe ya kukata na shoka.
Mmoja wa waandalizi wakuu wa harusi hiyo Aaltonen Jumba kutoka Slique Events Planner Limited, hata hivyo anasema ni vigumu kujua hasa ni kiasi cha peza zilitumiwa kuiandaa.Kuna waliotoa mahema, wengine viti na wengine magari ya kifahari.
Lakini Bw Jumba anasema wanaokosa sherehe
hiyo wamekosa kutambua na kufahamu vyema mambo ambayo yamekuwa yakijiri.”Wawili
hao tayari wamesaidiwa kifedha. Wamepewa shamba la kisasa, wakalipiwa fungate
na wameahidiwa pesa za kutumia kama mtaji kuanzisha biashara,” alisema.
Kwa sababu yote yameshughulikiwa, mbona
tusiwape kile ambacho walikosa? Kila mtu hutamania sana kuwa na sherehe kubwa
ya harusi.
credit.BBC Swahili
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U