NILIPOISHIA…
Visa vilianza vya kila aina, sijui
alipatwa na nini Minza aligeuka sana , nikawa nikimuuliza kitu ananijibu kwa
jazba, mara anaanza tu kunifokea kama mtoto mdogo. Kuna siku nilichukia sana na
mimi hasira zikanishika.
ENDELEA NAMI…
Nilifura hasa kama mtu ambaye amemfumania
mchepuko na mumewe, nilikuwa tayari kumvaa Minza kwa namna yoyote ile iwe kwa
maneno, michambo na hata ngumi ila wakati nataka kumfuata mahali alipokuwa
amekaa, ghafla nilisikia hodi, nikashindwa kuendelea na safari yanngu na kutega
masikio kusikia ni nani ambaye alikuwa anagonga mlango.
Kumbe alikuwa ni rafiki yake Minza ambaye
alikuwa amekuja pale kwa ajili ya kusukwa, basi hapo ndipo ikawa ponapona ya
siku ile, ,kiukweli nilikuwa nimekwazika sana na nilikuwa tayari kwa lolote.
Siku zilipita nikiishi kiaina aina ya
Minza, ila niliona kabiasa kuwa sura yake ilikuwa imejaa hasira na chuki dhidi
yangu ila hakuweza kunifukuza moja kwa moja.
XXXXXXX
Nakumbuka siku hiyo niliondoka na kwenda
Kibaha mjini kwa miguu kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kupata japo kibarua
cha kuosha vyombo kwenye kimgahawa chochote ilimradi nipate japo pesa kidogo
yakujikimu mimi na mwanangu pamoja na kuchangia pale kwa Minza.
Sikufanikiwa kupata kibarua, kwa kuwa
nilikuwa nimechoka hasa , nidhamu ya woga na mshipa wa aibu ulinikatika kabisa
nikaamua kugeuka kuwa ombaomba, nilifanya hivyo ilia angalau nipate pesa ya
nauli ya kunirudisha kijijini ila nilifanikiwa kupata pesa kama shilingi 350
ambayo ilinibidi nitafute chakula nikala na nikamnunulia mwanangu ndizi,
nikamlisha.
Niliporudi nyumbani Minza hakuwa ananijali
kwa lolote kwani aliendelea kuamini kuwa mimi ni mzigo kwake, basi akaamua
kuniambia kuwa natakiwa nijiandae hivi karibuni mpenzi wake anakuja?
Je,
Kecho atachukua maamuzi gani baada ya kuambiwa mpenzi wa Minza anayelipia kodi
ya nyumba na kumtunza kijijini hapo, anarudi?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U