Friday, February 3, 2017

Published 2/03/2017 02:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-28



 
NILIPOISHIA..
Nitaenda kwanza porini ila nikirudi nitakupeleka pale kibaha ilia uanze masomo hayo ya QT, Kibaha itakuwa ni karibu na nyumbani hivyo hautasumbuka sana. Tulikubaliana na yule kaka akarudi tena porini.
SONGA NAMI…

Barabara nzima ilikuwaimetapakaa damu, ubongo wa mtu ukiwa umemwagika, umati wa watu wanaoishi kando kando ya barabara ya KWA Mfipa wakiwa wamerundikana barabarani kushuhudia tukio la ajali lililopelekea watu au mtu kufariki dunia.

Lilikuwa ni tukio la ajali ambayo ilionekana kutisha sana hadi wakati huo sikuwa nimefahamu ni nani na nani ambaye alikuwa amepata ajali hiyo na kufariki dunia. Sikushangaa sana kutokana na eneo hilo kusifika sana kwa watu wengi kugongwa na kufariki papo kwa papo.
Tulizoea sana mara nyingi ajali inapotoea watu wengi hueleka barabarani kwa ajili ya kuangalia ajali ili kujioneka kama kuna mtu ambaye atamfahamu, wengine hutumia fursa hiyo kuwaibia wahanga wa ajali kwa kuwasachi na kadhalika.
 
Mimi pia nilikuwa ni miongoni mwa wale ambao walikuwa wanapenda kwenda kuangalia matukio hayo ya ajali pindi yalipotokea, nakumbuka siku hiyo mwili wangu ulikuwa kama mzito hivi, pamoja kusikia mlio wa matairi yakisugua lami kuashiria kuwa kulikuwa na ajali, bado sikuwashawishika kutoka wala sikusumbuka nayo kama zilivyo ajali zingine.

 Nikiwa sina hili wala lie, ghafla alitokezea jirani yetu namkuniambia Kecho twende bana tukashuhudie pengine hata unaweza kukuta ni mtu ambayo unamfahamu ukamsaidia, niligomagoma lakini alinivuta kwa nguvu yule dada na mimi kujikuta nikiunga tela kwa kukimbia.
Mamaa yangu, sikuamini macho yangu kwa kile nilichokiona, sikuweza kuvumilia zaidi ya kulipukwa na kilio cha sauti ya juu. Mama yanguuuu jamani Jakobo, jamani Jakobo weeeeee!

 Kila mtu alibaki akinishangaa mimi, wengi walitaka kujua nini kinachoniliza, je, nina undugu wowote na marehemu?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U





      edit