Friday, February 3, 2017

Published 2/03/2017 12:00:00 PM by

HANIAMINI HADI ANIPE MIMBA!


Naitwa Halima, mkazi wa Mkoa wa Tunduma, kwanza napenda kukupongeza sana kaka yangu G kwa kuwa msaada na mshauri mzuri wa masuala ya mapenzi, kwani nimekuwa nikifuatilia sana makala zako.

Mimi nina miaka 24, nina mchumba ambaye yuko  chuo mwaka wa mwisho, kama Mungu akipenda basi tunaratajia kwendqa kujitambulisha kati ya mwezi 7 mwaka huu.

Tatizo mpenzi wangu haniamini, anahisi nitamuacha, hivyo ameomba eti hadi anipe ujauzito ndiyo ataamini kuwa stamuacha, yaani anataka akajitambulishe nikiwa nina mimba  yake.

Kutoka moyoni mwangu, nampenda sana ila hajiamini, anahisi nitamwacha, kiukweli suala la kunipa mimba linaniweka njia panda sana, au nikubali anipe ujauzito ili ajue nampenda na sitamuacha. Naomba ushauri wako, nifanyaje?

Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI, MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U




      edit