NILIPOISHIA…
Ikiwa nimepita siku moja baada ya Minza
kuondoka, nikiwa niko nyumbani na mwanangu nakoroga uji, mara nilishangaa
vijana watatu wakawa wameniibukia tu vupu! Sikujua ni wapi ambapo walikuwa
wametokea kwani sura zao kwangu zilikuwa ni ngeni kabisa.
ENDELEA NAMI…
Nilishtuka sana kwani walionekana siyo
watu wema kwangu, niliwakaribisha lakini hawakuitikia zaidi ya kuonekana
wakiangaza huku na huku kama vile kuna jambo wanataka kulitekeleza kisha
watokomee, hofu iliendelea kunishika moyoni nwangu, nikajiuliza ni nini ambacho
kimetokea, nini wanachohitaji wale vijana kutoka kwangu.
Kijana mmoja alinisoegelea na kuniambia
kuwa leo lazima nilipe gharama ya muda wote wa kukaa na kulelewa na Minza kwa
sababu nilikuwa napenda kula vitu vya Minza bila kujua alikuwa anapewa na nani,
basi wao ndiyo walikuwa wakimuwezesha kwa maisha ya pale, Kwa Mfipa.
Nilistuka sana na kushindwa kuelewa, mbona
hilo suala Minza hakuwa ameniambia mapema, na kama ni hivyo mbona hata na mimi
nilikuwa nachangia siku moja moja, hasa wakati mpenzi wangu akiwa hai, nilianza
kuetetemeka mwili mzima nisijue cha kufanya.
Nilishangaa kuona vijana wawili wakianza
kunishika nguo zangu huku mwingine akitaka kama kunishika mdomoni kwa ajili ya
kuniziba mdomo ili nisipige kelele.
Nililia kwa uchungu sana huku nikijitetea,
ghafla nilisikia sauti ya kijana mwenzao akiwataka waniachie, nikaanza
kujitetea kwa kueleza matatizo yangu niliyoyapitia hadi kufika hapo nilipo kwa
Minza, vijana wawili walionekana kutokujali, na kuahidi kuwa siku hiyo walikuwa
lazima wanibake kama ambavyo wameagizwa na rafiki yangu.
“Oya mwana unazingua tumalize bhana
twende, mwisho kitasanuka,”alisema kijana mmoja ambaye sauti yake ilisikia kama
ya mvuta bangi sugu.
Yule kijana aliyekuwa ananitetea
akawaambia hakuna wasifanye chochote, kisha akawauliza “Kama wewe huyu dada
angekuwa ni ndugu yako wa damu ungeweza kumfanyia kile ambacho tunatakiwa
kukifanya? Ebu tuachane na ujinga huu washikaji,” alisema yule kaka.
Moyo wangu kwa mbali ukaanza kupata ahueni
na kuanza kupumua vizuri kidogo. Lakini wale vijana wawili wakaendelea
kung’ang’ania tu kunibaka, kwa kuwa walikuwa wamelipwa kwa ajili ya kazi hiyo
ina maana kama watashindwa kunibaka basi itabidi warudishe pesa kwa wajiri wao.
Kiukweli nilishangaa, Mungu wa ajabu kwani
wao wenyewe wakaanza kubishana na kutofautiana kabisa, wengine wakitaka
wanibake, huku yule kaka mmoja akionekana kupingana nao na kunitete kwa nguvu
zote.
Ghafla yule mkaka aliyekuwa ananitetea
aliingiza mkono mfukoni kisha akatosa kitu, ambacho sikuwa ni nimekifahamu ni
nini kabla.
Je,
unataka kufahamu yule mbakaji mwema alitoa nini? Usikoese kesho muda kama huu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U