Mimi ni binti ambaye nina mahusiano na kijana mmoja,
tuna muda kidogo kwenye mahusiano yetu lakini hivi karibuni nilimfumania akiwa
na mwanamke mwingine.
Niliumia sana, kwani ni mwanaume ambaye nimekuwa
nikimwamini na kumkubali. Aliniomba msamaha na kuahidi kuwa hatorudia tena kwa kuwa
na mimi nina mpenda sikuona sababu ya kutokumsamehe ili maisha yaendelee.
Siku zilipita hatimaye nikaja kubaini kuwa mpenzi
wangu bado anaendelea na yule mwanamke ambaye nilimfumania naye, nikimuuliza
anakataa. Nimeumia ni kama amenitonesha kidonda change ambacho kilikuwa
kimeanza kupona.
Sijui na kufanya maana akili yangu imechanganyikiwa,
naomba ushauri wako kama umebahatika kusoma ujumbe huu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U