Friday, February 24, 2017

Published 2/24/2017 02:00:00 PM by

NAMNA YA KUONDOKANA NA HOFU





HOFU ni hali ya mtu au kitu kuogopa kitu au jambo fulani, aidha kwa kuona labda yeye ni dhaifu kuliko mtu mwingine au jambo husika au kwa kuhisi tu kuwa hawezi kufanya jambo fulani lakini kumbe kiuhalisia angefanya na jambo lingefanikiwa.

Hofu ziko za aina nyingi kuna, hofu ya kuzaliwa nayo, kurithishwa au kurithi au kutengenezewa.

HOFU YA KUTENGENEZWA

Hofu hii inaweza kuwa ni ya kusikia, kuona au kusimuliwa kuwa jambo fulani ukilifanya huwezi kufanikiwa kwa sababu ya kadha wa kadha kwa mfano:

Hofu yako inakuambia kuwa huwezi kuwa kiongozi wa mtaa, kijiji, wilaya, mkoa, au taifa eti kwa sababu mzazi wako hajawahi kuwa.

Kisa kwenye ukoo wenu hakuna historia ya mtu kuwa kiongozi hivyo unaamini kuwa historia yako inakuhukumu, inakuondolea sifa za kuwa kiongozi wa sehemu au jambo fulani.
Jambo ambalo halina ukweli wowote, na kwa mtu mwenye kuthubutu hujaribu kuivunja roho hiyo (ya kuhisi kuwa kwenye ukoo wenu hakujawahi kutokea mtu wa hivyo), ili kuifanya familia au ukoo wake nao kuingia kwenye orodha ya viongozi ambao watakuwa wanatajwa na waoga wengine.

Watu huamini mtu mwenye mali au pesa nyingi labda ni mtu mwenye bahati zaidi kuliko wengine, wengine huhisi labda mtu huyo ni mwema sana mbele za Mungu na ndiyo maana katunukiwa mali hizo jambo ambalo si kweli kila kitu kinatafuta lakini cha kujifunza KUNA WENGINE WANAPESA AMBAZO SI ZA HALALI WAMEWAUMIZA WENZAO ILI WAO WAWE NA PESA NA WAHESHIMIKE.

Yawezekana ukoo au familia yake haijawahi kufanya jambo fulani kubwa kiasi cha familia husika kupongezwa na wanajamii wanaowazunguka.

Hii ni hofu mbaya, hofu ambayo hata kama una elimu kubwa kiasi gani lakini bado inakutafuta na kuivunja hofu hii ni kuwa na uthubutu wa ndani yako.

Hofu ya kuhisi wewe huna nguvu ya kufanya jambo fulani, huwezi kwa sababu huna pesa, elimu, huna nguvu, huna jina lolote wala heshima yoyote kwenye familia, ukoo au kijijini kwako basi huwezi kufanya jambo hilo.
Usikose sehemu inayofuatia ya mada hii…

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
      edit