NDUGU zangu, linapokuja suala
la kutafuta maisha mazuri na yenye mafanikio, wapo watu ambao wanadiriki
kujiingiza katika shughuli zisizo halali ambazo mwisho wa siku zinaweza
kuyahatarisha maisha yao.
Lakini niwakumbushe tu kwamba, zipo
kazi nyingi tu ambazo ukizifanya kwa nguvu zote na kwa malengo unaweza
kuwa na mafanikio makubwa na ukaishi maisha ya furaha na amani. Hapa
nazungumzia zile kazi ambazo ni halali.
Lakini huwa najiuliza, hawa wanaofanya kazi zisizo halali walishawahi kujiuliza hatima ya maisha yao itakuwaje?
Kwa nini ufi kie hatua ya kufanya kazi
ambayo itafanya maisha yako yawe hatarini? Wapo wanaosema eti wanafanya
hivyo kwa sababu maisha ya sasa ni magumu na hivyo ugumu huo wa maisha
unaweza kuukabili kwa kufanya kazi hizo.
Hii ni hatari sana na hata hao
wanaojipatia mapesa kwa kufanya kazi kama vile za kuuza madawa ya
kulevya, bangi, utapeli, uchangudoa na shughuli nyingine za namna hiyo
maisha yao si ya furaha kama watu wanavyodhani. Wanaishi maisha ya
wasiwasi huku wakihofi a usalama wa maisha yao.
Uchunguzi unaonesha kwamba wengi
wanaofanya biashara hizo haramu mwisho wao huwa mbaya sana ambapo baadhi
yao huishia kuuawa, kufa ama kufungwa jela.
Nenda kwenye magereza leo hii utakuta
waliojaa huko wanatuhumiwa kwa ujambazi, wizi, uuzaji wa madawa ya
kulevya, watu ambao walidhani kwa kufanya hivyo wanaweza kuyafanya
maisha yao yakawa mazuri kumbe ndiyo wanajiweka katika wakati mgumu
zaidi.
Mimi nadhani zipo kazi nyingi tu ambazo
unaweza kuzifanya na ukawa tajiri ama kuwa na mafanikio makubwa bila
kuiba kitu cha mtu wala kudhulumu. Kwa kutumia akili yako, nguvu zako
pamoja na maarifa aliyokujaalia Mungu naamini unaweza kufanikiwa na
kuishi maisha ya amani yaliyojaa furaha tele.
Siyo mpaka uibe ndiyo unaweza
kufanikiwa, siyo lazima uuze madawa ya kulevya wala kuuza mwili wako
ndiyo ufanikiwe. Fahamu kwamba wapo watu wengi waliopata mafanikio
makubwa kwa kupigana kihalali.
Hivi unadhani watu mabilionea na wenye mafanikiio makubwa duniani
walifi kia hatua hiyo kwa njia za mkato? La hasha! Hao walitumia akili na nguvu zao katika kuusaka utajiri huo.
Siku zote ukae ukijua kwamba maisha
hayana njia ya mkato. Kwa maana hiyo basi wanaoendesha maisha yao kwa
njia ya mkato, hawana furaha na mafanikio ya kweli katika maisha yao.
Kimsingi wanaotegemea kuendesha maisha
yao kwa kufanya kazi ambazo siyo halali wako kwenye nafasi nzuri ya
kukumbwa na balaa katika maisha yao kiasi cha kuwafanya kutozifurahia
fedha walizonazo.
Wapo akina dada ambao wameridhika
kuendesha maisha yao kwa kufanya biashara ya kuuza miili yao. Wanaofanya
hivyo wanaeleza kwamba kinachowasukuma kufanya hivyo ni ugumu wa
maisha.
Maisha yanaweza kuwa magumu kama hutajishughulisha.
Lakini hata kama maisha ni magumu kiasi gani ndiyo ufi kie hatua ya kuweka rehani maisha yako?
Asikudanganye mtu wengi wanaofanya
biashara ya uchangudoa maisha yao yako hatarini hasa kipindi hiki
ambacho ugonjwa wa Ukimwi unasumbua kila kona ya ulimwengu.
Labda nihitimishe kwa kusema kwamba,
kuna kila sababu ya kubadilika na kuangalia njia sahihi za kuendesha
maisha yetu. Tuachane na tamaa zisizo na msingi na kutaka kujipatia
fedha kwa njia za makato. Tuelewe kwa kufanya hivyo hatuwezi kupata
mafanikio ya kweli na tutakuwa tunayahatarisha maisha yetu.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza HapaNa.M&U
CHANZO: GPL