Asikwambie mtu unapoanza
kufanya jambo Fulani kuna watu ambao watakucheka na kukudhihaki na kadhalika.
Lakini siku zote jifunze kuamini katika mawazo yako, acha wakucheke, vicheko
vyao vifanye ni kama kuni ambayo
inakuchochea wewe kwa kukuchoma ili uendelee kuumiza kichwa na mwisho wa
uweze kufika malengo yako.
Nilizungumzia mambo kadhaa
ambayo kama utayaweka nia basi una
nafasi kubwa sana ya kufikia malengo. Nilizungumzia kuhusu dhamila yenyewe,
malengo.
Leo nitazungumzia mambo
mengine mawili ambayo ni ya muhimu sana kuyazingatia ambayo ni:
1. KUJITUMA
Kujituma
ni siri kubwa sana kwenye kila jambo katika maisha ya mwanadamu, basi ukijituma
unaweza kufikia malengo yako vizuri sana kama ni kazini unaweza kupandishwa
cheo au mshahara kwa sababu ya uwezo wako wa kujituma, siyo mtu wa kusukumwa,
unafanya kazi kwa mujibu wa sheria za kazi.
Kujituma
kuna kufanya kuendelea kuwa bora zaidi kwani hata kama kampuni Fulani
itakuachisha kazi basi ni rahisi kwa wewe kupata nafasi kwenye kampuni nyingine
kwa sababu yawezekana sifa zako za kujituma zilishasambaa siku nyingi pasipo
wewe kufahamu.
2. HESHIMA
Ni lazima
uwe na heshima kwa wateja wako, wafanyakazi wenziyo na hata nviongozi. Heshima
nyingine ni kwenye matumizi na matunzo ya pesa, hata kama unaingiza kipato
kikubwa kwa siku na hata faida yako inakuwa ni kubwa kuliko mtaji basi kuwa
naheshima na faida hiyo. Kwani kama utakuwa na mambo matatu niliyoyataja juu
lakini hauna heshima yaani ni mfujaji wa mali au pesa basi huwezi kufikia
malengo yako.
Heshima
nia pamoja na wale wote wanaokusaidia katika kukamilisha shughuli yako awe
mlinzi, mtumishi wa ndani, muhudumu, mtu wa mapokezi na wengineo.
Mpenzi mwanaM&U
naaamini kuna jambo utakuwa umelipata kupitia mada hii ya ujasiriamali, kikubwa
ni wewe kukifanyia utekelezaji wake. Achana na mambo ya kusuburi mtu mwingine
aje kukusaidia kufikia malengo yako, hilowazo ondoa kichwani kwako kwani
mwanadamu hana uhakika wa kuimaliza siku yake akiwa salama, hivyo unaweza
kumtegemea lakini akakuangusha kwa kusudi au kwa jambo lililo juu ya uwezo
wake.
Siku zote nimekuwa
nikisema kuwa kama una wazo, maono, au jambo unahitaji kulifanya basi anza sasa
haujachelewa, suala la umri wako kwenda siyo ishu, siyo tatizo kabisa, acha
wengine wacheke ila mwisho wa siku watakusalimia kwa heshima.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
MWISHO