2-MALENGO
Ili dhamila yako ikamilike
ni lazima iende na.malengo ya jambo husika haijalishi malengo yako yatakuwa ni
ya pesa nyingi, kazi au ndoto kubwa, cha kufanya ni kuwa na malengo nayo.
Malengo hayo yanaweza kuwa
ni ya muda mfupi kwa maana ya miezi 3, malengo ya kati, miezi 6 au malengo ya
muda mrefu yaani miezi 12, mwaka na kuendelea.
Unapokuwa na malengo
yanakusaidia kuhalikisha unafikia dhamila yako, mfano unadhamila ya kumiliki
shule ya msingi au chekechea na una kiwanja cha nusu heka au heka moja, basi weka malengo ya kuhakikisha unajenga
darasa moja la kuanzia.
Kwa kufanya hivyo ni
lazima utajibana kwa hali na mali ili uweze kuchimba msingi, kumwaga mawe na
hatimaye kuanza kupandisha chumba hicho.
Ni.lazima uwe na lengo ili
uweze kufika unapotaka kufika kama hauna utakomea kulalamika kila siku na
kuwaona wenzako wanaendelea.
Hao unaodhani wana pesa
nyingi ndiyo maana wanaendelea si kweli kuwa wana magunia ya pesa bali wana
dhamila na malengo ya dhati kutoka mioyoni mwao.
Pamoja na kuchelewa kwako
kuanza kuwa na malengo hata hivyo bado una nafasi ya kuanza sasa, jitathimini,
jitambue, thubutu na kile unachodhani ni kipaumbele chako.
Usikose sehemu ya pili ya
mada hii siku ya Alhamisi.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U