Friday, April 7, 2017

Published 4/07/2017 02:00:00 PM by

MASHETANI YA ZIMAYA-2





ILIPOISHIA…

Ilipofika saa 12:30, Matrida alimaliza usafi wake wa nje na kubakiwa na usafi wa ndani, wakati akijiandaa kuingia ndani, akiwa bado yupo mlangoni amekaa kwa uchovu wa kazi ya siku hiyo akiwa anafikilia kufanya kazi iliyo baki lakini pale alipokaa kama hatua tatu kuna kitu alikiona mbele yake.

SONGA NAYO

Kumbe alikuwa ni ndege aina ya njiwa mwenye  rangi tatu, bluu, kijani na nyeupe, ukweli ndege yule alimvutia sana Matrida.

Ndege yule alionekana nakitembea kwa kuchechemea kuashilia kuwa mguu  wake mmoja ni mbovu, Matrida alimuonea huruma yule ndege, alimchukua na kuingia naye ndani na kumuweka chumbani kwake, alimpa maji njiwa yule na kumtafutia nafaka kwa ajili ya chakula.
Ilipofika saa 1:15 asubuhi wakati akiendelea kumpa chakula ndege yule, huku akiendelea kumuuliza maswali mbalimbali “Wewe ndege kwa nini upo hapa?  Umeumia hivyo na umetokea wapi?” Kama ilivyo kawaida ya mtoto ziku zote, alizidi kumuuliza yule njiwa “Hutaki kunijibu si ndiyo, basi mimi sitakuwa rafiki yako.”


Baada ya Matrida kumuuliza ndege yule maswali mengi, yule ndege alitoa sauti na kusema: “Sikuwahi kupata rafiki kama wewe Matrida, asante sana kwa msaada wako, umenijali sana, kwa kunipa chakula na maji.” Ndege aliruka na kumponyoka Matrida. Matrida akabaki kumtazama yule ndege hadi akapotea machoni mwake.

Ilipotimia saa saa 2:00 asubuhi, mama na baba yake Matrida walikuwa wameshaamka na kukuta Matrida amemaliza kazi zote. Ilipofika saa tano asubuhi ni muda maalumu wa baba na mama yake Matrida kuelekea kazini, Matrida alikuwa ameketi kwa nje, baba na mama wapotoka nje wakamkuta Matrida akicheza, mama alimwambia Matrida “Sitaki ucheze nje ukaacha mlango ukiwa wazi embu nenda  ukakae ndani.” 


Matrida alipoambiwa vile akasema “ Mama muda wote nikae ndani tuuuuhh, aahh!!!  Mimi nipo hapa nacheza” mara baba alikerekwa, alimpiga kibao Matrida baada ya kumjibu vile mama yake na kumwambia.


Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit